31.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Wastara alamba dili nono

Wastara Juma
Wastara Juma

Na CHRISTOPHER MSEKENA,

NYOTA inawaka! Diva wa filamu za Kibongo Wastara Juma, amepata dili jipya baada ya kusaini mkataba utakaomwingizia fedha nyingi.
Mkataba aliosaini Wastara ni wa kuwa balozi wa simu ya KZG ambayo hutengenezwa na Kampuni ya KZG kutoka China, ambapo atakuwa na uhakika wa kulamba milioni 400 kwa mwaka.

Tukio la kusaini mkataba huo lilifanyika Septemba 28, mwaka huu katika Hoteli ya Demag iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam ambapo atafanya nao kazi kwa muda wa miaka miwili.

Kwa muda ambao staa huyo atafanya kazi na kampuni hiyo, atakuwa na uhakika wa kuingiza kiasi cha shilingi milioni 800 kwa muda miaka miwili, fedha ambazo ni wastani wa shilingi milioni 33 kwa mwezi.

Akizungumza muda mfupi baada ya kusaini dili hilo, Wastara alisema: “Nashukuru sana Mungu kwa kupata mkataba huu, naamini hii ni kutokana na kazi zangu nzuri na ushirikiano na mashabiki wangu. Naamini bila mashabiki wangu kunikubali, ubora wangu usingeonekana.”

Baadaye kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, alitoa taarifa hizo kwa mashabiki wake kwa kueleza furaha yake baada ya kupata dili hilo.

“Alhamdulilah leo tarehe 28, nimesaini rasmi mkataba wa kuwa balozi wa kampuni ya uuzaji wa simu ya China KZG. Kuanzia leo mimi Wastara Juma Issa nimeanza rasmi kazi ya Ubalozi wa KZG itakayoniingizia milioni 400 kwa mwaka,” aliandika Wastara kupitia ukurasa huo.
Wastara ameshiriki filamu nyingi zilizomuweka juu kisanii, baadhi yake ni pamoja na Mboni Yangu, 2 Brothers na Briefcase.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,625FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles