29.3 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Wastaafu washauriwa kuachana na mikopo umiza kulinda mafao yao

Na Malima Lubasha, Serengeti

Watumishi Wastaafu serikalini wilayani Serengeti mkoani Mara, wametakiwa kujiepusha na mikopo umiza pamoja na kuoa wake wengi baada ya kupata mafao ya kustaafu hali ambayo inaanzisha migogoro ya kifamilia na kuwarudisha kwenye dimbwi la umasikini.

Ushauri huo umetolewa na Meneja Mwandamizi Kitengo cha Mikopo Benki ya Posta Tanzania (TPB) Joanitha Deogratias wakati akitoa elimu ya mikopo nafuu kwa watumishi wastaafu Serikalini wilayani hapa ili waweze kupata mikopo kupitia Benki hiyo kuboresha maisha yao.

Deogratias alisema kuwa Benki hiyo kwa kuenzi michango ya wastaafu waliolitumikia Taifa,Benki ya TPB kwa kushirikiana na mifuko ya hifadhi za jamii ma wizara ya fedha imeamua kutoa mikopo maalumu ili kuwawezesha wastaafu waweze kukidhi mahitaji yao muhimu na kuwaokoa kupitiwa na janga la matapeli wa mikopo umiza. 

Alisema Benki hiyo ni mali ya serikali hivyo mikopo inayotolewa inakusudia kuwawezesha kupata kiasi cha fedha kulingana na kiwango cha malipo ya pensheni yake ya kila mwezi ili waweze kuboresha maisha, kukidhi gharama za matibabu na ada za shule pamoja na kusaidia kuendesha shughuli za kiuchumi kwa kuanzisha miradi mbalimbali.

Aidha, Deogratias aliwaonya wastaafu kuachana na tabia ya kwenda kuongeza mke mwingine pale wanapopata mafao ya kustaafu kwani hayo siyo matumizi sahihi ya fedha na imekuwa ndio chanzo cha migogoro ya kifamilia na wengine kujiingiza katika mikopo umiza.

“Sisi kama Benki ya Serikali tunaona hali hii haikubariki kulingana na umri mlionao ni dhahiri nguvu zimepungua, ndiyo maana tunapita kila wilaya kutoa elimu kwa wastaafu ili waweze kukopa fedha kupitia TPB, acheni kuoa, achaneni na mikopo umiza, tumieni taasisi za kifedha za serikali kupata mikopo nafuu,”Alisema Deogratias.

George Mazeleng’we Afisa Mwelimishaji kutoka Benki  hiyo alisema alisemaya mikopo inayotolewa kwa wastaafu itumike kwa malengo sahihi ili kunufaisha familia kwa kuanzisha biashara, kilimo, ufugaji na ujenzi wa nyumba.

Alisema muombaji anaweza kukopa kiwango chochote kulingana na mafao yake hata zaidi ya Sh.Milioni 100 kipindi cha kurejesha mkopo ni kati ya mwaka mmoja hadi miaka 6 kutegemea umri wa mwombaji pia benki inatoa mikopo makundi yasiyo rasmi,vicoba,kidini,vikundi katika makazi na maeneo ya kazi.

Chama cha Watumishi Wastaafu Serikali Serengeti(CHAWASE) chenye wanachama Zaidi ya 200 wakichangia maoni yao walishauri Serikali kuwaongezea kiasi cha fedha katika pensheni ya kila mwezi kwa kuwa wengi wao  wanapata kiasi kisichotosheleza ingawa wamelitumikia taifa kwa moyo na uadilifu mkubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,220FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles