26.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Wastaafu wahimizwa kujikita kwenye kilimo

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Mkurugenzi wa kampuni ya Namburi Agricultural Company, Dk. Mary Mgonja, amewataka wastaafu nchini kutumia muda wao kuingia kwenye kilimo ili kuendelea kufanya kazi na kujiimarisha kiafya na kiuchumi pia.

Akizungumza na Mtanzania Digital leo, Agosti 2, 2024, katika maonesho ya Kitaifa ya Kilimo Nanenane yanayoendelea jijini Dodoma, Dk. Mary alisema kampuni yao imekuwa ikizalisha mbegu bora zinazohimili ukame na zinazoendana na aina zote za ardhi.

“Wakulima nchini wanatakiwa kutumia mbegu zinazozalishwa nchini ambazo zinaviwango na zinahimili ardhi aina zote. Hapa tunazo mbegu zinazohimili ukame ambapo mkulima wa maeneo hayo anaweza kuzitumia na kufanikiwa kuvuna vizuri na kufanyabiashara,” alisema Dk. Mary.

Aidha, Dk. Mary aliipongeza Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Taasisi ya Udhibiti wa Mbegu Bora Nchini (TOSCI) kwa juhudi zao za kuitangaza nchi na kuzuia uuzaji wa mbegu bandia.

“Nitoe rai kwa wakulima kuwa makini wakati wa kununua mbegu na kuhakikisha mbegu hizo zina alama ya TOSCI,” alisisitiza Dk. Mary.

Aliongeza kuwa kampuni ya Namburi inafanya shughuli zake za uchakataji na uzalishaji katika mkoa wa Songwe lakini wanasambaza mbegu zao kwenye maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha kila mkulima anapata mbegu hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles