23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wasomalia kuziamua Taifa Stars, Malawi

1264922_heroaNA ABDUCADO EMMANUEL, DAR ES SALAAM

WAAMUZI kutoka nchini Somalia wamepangwa kuchezesha mechi ya hatua ya awali ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi kati ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na Malawi ‘The Flames’ utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam keshokutwa.

Mtandao wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kuhusu mchezo huo namba 13 kanda ya Afrika, umeonyesha kuwa mwamuzi wa kati atakayepuliza kipenga atakuwa ni Haji Wiish.

Mwamuzi msaidizi namba moja anatarajia kuwa ni Hamza Abdi, mikoba ya msaidizi namba mbili itashikwa na Salah Omar, huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Bashir Olad.

Tayari kikosi cha Stars kimeshaanza maandalizi ya mchezo huo tokea Ijumaa iliyopita chini ya Kocha Mkuu Charles Mkwasa, Msaidizi wake, Hemed Morocco na Kocha wa Makipa, Peter Manyika.

Kuhusu ujio wa wachezaji wanaocheza soka la kulipwa, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Celestine Mwesigwa, aliliambia MTANZANIA jana kuwa wote watawasili leo.

“Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe), wao wanamalizia mechi yao leo (jana) ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kesho (leo) watatua nchini hata Mrisho Ngassa naye tunamtarajia kesho (leo),” alisema.

Wakati huo huo, timu ya Malawi imewasili jana asubuhi nchini ikiwa na msafara wa watu 26 wakiwemo wachezaji 20 wa kikosi hicho wakiwa tayari kabisa kuivaa Stars.

Mchezo wa marudiano utafanyika Malawi kwenye Uwanja wa Kamuzu Jumapili hii na bingwa wa jumla atafuzu kwa raundi wa pili kwa kumenyana na Algeria kabla ya kutinga hatua ya makundi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles