29.2 C
Dar es Salaam
Friday, August 19, 2022

Wasiosikia walilia lugha ya alama

RAMADHAN HASSAN-CHAMWINO

KATIBU wa Chama cha Viziwi Mkoa wa Dodoma (CHAVITA), Amina Issa amesema kukosekana kwa mawasiliano ya lugha ya alama kunasababisha wenye ulemavu wa kutosikia kukosa haki zao za msingi.

Hayo yalielezwa mwishoni mwa wiki na katibu huyo   alipozungumza na waandishi wa habari kuhusiana na umuhimu wa mawasiliano ya lugha ya alama kwa watumishi wa serikali.

Alisema changamoto ya kukosekana kwa lugha hiyo ya alama  kunawafanya kuendelea kukosa mahitaji yao muhimu kwenye sekta hizo kama wanavyopatiwa watu wengine wasiokuwa na ulemavu.

“Tunaiomba serikali kutenga bajeti kwa ajili ya watumishi wao   waweze kujifunza lugha ya alama ambayo itawawezesha kuwa na mawasiliano na sisi   tunapohitaji kupatiwa mahitaji mbalimbali kwenye taasisi husika zikiwamo za benki, hospitali, mahakamani, polisi na  katika majengo ya serikalini,” alisema .

 Amina aliwataka vijana wa chama hicho cha viziwi Mkoa wa Dodoma kuunda vikundi  waweze kukopeshwa na taasisi za  fedha zitakazowawezesha kujiinua  mapato zaidi badala ya kutegemea ufadhili ambao hauna uhakika kwa asilimia kubwa.

Kwa mujibu wa Amina,  wakiungana   itakuwa rahisi  kuibua miradi ambayo itakayoweza kuondokana na dhana ya utegemezi kwa watu na wafadhili ambao kwa asilimia nyingi umekuwa ukiwafanya kuwa masikini.

Alisema  hivi sasa serikali imetoa fursa nyingi za kujiajiri wenyewe ikiwamo na vitambulisho ambavyo vitafanya kufanya shughuli mbalimbali za kujipatia kipato bila kubugudhiwa watakapokuwa na vikundi hivyo vya ujasiriamali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,987FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles