24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WASIOKUWA NA VITAMBULISHO VYA TAIFA MARA KUSAKWA

Na SHOMARI BINDA


MKUU wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, amewaonya watu ambao wamekuwa wakikwepa   kujiandikisha vitambulisho vya taifa kuwa  baada ya   hatua hiyo kukamilika ataagiza polisi  kuwasaka waliopuuzia.

Alisema watu hao watatakiwa  waeleze sababu za kutojisajili na kupata vitambulisho.

RC alikuwa akizungumza juzi baada ya kumalizika siku 90 za usajili na uandikishaji wa vitambulisho vya taifa kwa Mkoa wa Mara.

Alisema hatua hiyo imekamilika kwa kusajili   wananchi 718,647 kati ya 763,142 waliostahili kusajiliwa hivyo kufanya idadi ya wananchi waliodahiliwa kufikia asilimia 94.

Alisema katika hatua hiyo pia wamesajili wageni wakazi 224 ambao wamekuwa wakiishi  halali mkoani humo.

Rc aliwaonya ambao hawakujiandikisha kutumia siku za marekebisho kujisajili na kujiandikisha.

“Wale waliojiandikisha baada ya hatua hiyo kumalizika watapata vitambulisho vyao na wasiokuwa navyo tutawahesabu kuwa siyo wenzetu.

“Zipo wilaya ambazo zimefanya vizuri katika hatua hii  ni Musoma na Bunda ambazo zimesajili kwa asilimia 112 zinastahili kupongezwa,” alisema.

Hata hivyo alisema licha ya kukamilika hatua hiyo   itaendelea katika ofisi za wilaya hivyo kuwaomba wale ambao hawakupata fursa hiyo wafike  kukamilisha kuanzia Mei hadi Juni 2018.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles