20.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Wasikie Simbu, Sulle na safari yao Tokyo Japan

GLORY MLAY-DAR ES SALAAM

RIADHA inarejea kwa kasi, baada ya kilio cha miaka mingi cha wapenzi wa michezo nchini, kutamani kuona mchezo wa huo unarudisha hadhi yake kama ilivyokuwa  1970.

Kureajea kwa heshima ya riadha Tanzania, kumenogeshwa na  taarifa njema za wanariadha wa Alphonce Simbu na Agustino Sule, kufuzu mashindano ya Olimpiki, yatakayofanyika mwakani Tokyo Japan.

Ni dalili tosha za kuonyesha kwamba Watanzania wanahitaji sasa, kuona wanariadha wao wakifanya vizuri katika michezo ya kimataifa.

Spotkiki  lilipata nafasi ya kufanya mahojiano na wanariadha ambao wanajianda kuelekea Japan, hapo mwakani, kujua siri na changamoto wanazokumbana kwenye maandalizi yao.

ALPHONCE SIMBU

Ni mwanariadha wa Tanzania, ambaye amekuwa wa kwanza kufuzu kwa michezo ya Olimpiki itakayofanyika jijini Tokyo Japan mwakani.

Simbu amefanikiwa kukata tiketi hiyo nchini Japan, baada ya  kukimbia muda mzuri katika Mbio za Lake Biwa Marathon, ambazo zinatambulika na zimepitishwa na Shirikisho la Riadha la Kimataifa (IAAF).

Katika mbio hizo zilizokuwa na ushindani wa hali ya juu kutoka kwa washiriki wa nchi mbalimbali, Simbu kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), na mshindi wa medali ya Shaba ya Dunia, alikamata nafasi ya sita akiandika rekodi yake mpya, akitumia saa 2:08.27.

Rekodi ya awali ya Simbu, kabla ya mbo hizo  ilikuwa ni saa 2:09.10, aliyoiweka London Marathon.

Kabla ya Biwa Marathon, Simbu alishiriki mashindano ya New York City Marathon, yalifanyika mwaka jana nchini Marekani, hata hivyo hakuweza kumaliza mbio  hizo za km 42 kutokana na tatizo la misuli alilokua nalo.

Baada ya mashindano hayo, alikaa nje  kwa muda mrefu na kushiriki Colombia Marathoni, mapema mwaka huu lakini hakuweza kufua dafu.

Simbu aliibuka bingwa kwenye mashindano ya Majeshi baada ya kukimbia km 21, Machi 8 mwaka huu, jijini Dar es Salaam, kabla ya kushuriki Biwa yaliompa tiketi ya kushiriki Olimpiki mwakani.

Siri ya mafanikio anasema ukiwa na malengo na kujituma kwenye mazoezi, ndio siri ambayo imemfanya kutangulia Olimpiki hapo mwakani.

“Mwanariadha ambaye anamalengo lazima ajitume kwa moyo na juhudi, bila hata kumtegemea kocha, hata nikiwa kazini nikipata muda nafanya mazoezi sisubiri mpaka niambiwe,

“Pia uwe na malengo na sio upo kwenye riadha kwa sababu na fulani yupo hapana, hii ni ajira kama zilivyo nyingine.

Changamoto anasema changamoto kubwa iliyopo ni ukosefu wa ufadhili, ambao utawawezesha wao kupata yale mahitaji wanayohitaji wakati wa maandalizi.

“Unaweza kukuta mwanariadha yupo kambini, lakini anaweza kula chai na mkate ili aendelee na mazoezi, mwanariadha kama huyo hawezi kwenda kushindana na wa Kenya, ambao wanapewa kila wanacho hitaji.

“ Tunawaomba wafadhili wawe wanajitokeza mapema kwani sisi tunahitaji kufanya maandalizi yenye viwango ambayo yatatufanya kuiletea Tanzania medali kwenye mashindano makubwa kimataifa au ya kitaifa,” anasema. Simbu

Ushauri anasema kama Tanzania inahitaji wanariadha bora, serikali inatakiwa kuwekeza kwa asilimia 100 ili kuhakukisha inarudisha heshima iliyokuwepo zamani.

“Wenzetu kama Kenya, Uganda na Ethiopia serikali zao zimewekeza moja kwa moja katika michezo, ndio maana mara nyingi wao ndio wanashinda, wanawekwa kambini kwa muda mrefu na wanapewa kila wanachohitaji.

“Watuangalie kwa mapana zaidi kwani na sisi tukistaafu kama wakina Bayi na Nyambui, wapatikane wengine kama hao ambao wataifanya Tanzania kusifika kila kona ya dunia,” anasema Simbu.

AGUSTINO SULLE

Mwanaridha wa kwanza kutoka klabu ya Taley ya jijini Arusha, ambaye amefanikiwa kufuzu mashindano ya Olimpiki.

Sulle kabla ya kushiriki mashindano hao, anashikilia rekodi ya Taifa Marathon ya Saa 2:07.45 aliyoiweka Toronto Marathon Canada mwaka jana, alishika nafasi ya 17 akitumia saa 2:12.42.

Muda wa kufuzu kwa Olimpiki, ambao unaanza kutambuliwa kuanzia Januari mwaka huu ni saa 2:14. kwa wanaume Marathon.

Katika mbio hizo, mshindi wa kwanza aliibuka Salah Eddine-Bounasr wa Morocco aliyetumia saa 2:07.52, akifuatiwa na Asefa Tefera wa Ethiopia 2:07.56, huku nafasi ya tatu ikienda kwa Stephen Mokoka wa Afrika Kusinia 2:07.58.

Matarajio yake Sulle anasema baada ya kufuzu Olimpiki, ataendelea kufanya mazoezi na kujituma, huku akushiriki mashindano mbalimbali ya kumuwezesha kuibuka medali ya dhahabu.

“Naendelea na mazoezi kwani hapa mbele tunamashindano ya kimataifa, ni kujipanga tu, ninaamini nitashinda hivyo tunaomba na wadau waendelee kutuunga mkono.

Changamoto anasema changamoto anayoiona yeye ni wadau kushindwa kuupa kipaumbele mchezo wa riadha, hivyo huwekeza kwenye soka kwa asilimia kubwa.

“Wadau wengetambua kuwa riadha ni moja ya ajira zinazolipa wasingekuwa wanaacha, riadha ni ajira tunaona watu wanajenga nyumba na wanakuwa na maisha mazuri kupitia mchezo huu, wanatakiwa wauangalie kwa upana zaidi,” anasema Sulle.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,595FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles