22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

Wasichana watakiwa kujitambua ili kutimiza ndoto zao

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Wasichana wametakiwa kujitambua, kujiamini, kukataa vishawishi na marafiki wabaya ili kuweza kutimiza ndoto zao walizojiwekea.

Hayo yameelezwa Ijumaa April 30 mwaka huu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. John Jingu wakati akifunga mkutano wa mwaka wa wadau wanaotekeleza afua za VVU na Ukimwi zinazowalenga wasichana balehe na wanawake vijana.

Katibu Mkuu huyo amewataka vijana kujitambua na kujiamini kwani ni nyenzo muhimu katika kutatua Changamoto zinazoendana na umri wao.

“Naomba wasichana mjitambue na kujiamini kwani ni nyenzo muhimu ya  kutatua Changamoto zinazoendana na umri wenu.Jiamini unaweza kupambana na changamoto,ukilegea kidogo ukiteleza unaharibu ramani ya maisha yako.

“Anakuja Sponser anakuimbia nyimbo zote na wewe unaingia mkenge unapata maambukizi ya Ukimwi unapata mimba niambie maisha yatakuwa sawa hapo? Lakini ukijitambua hautakubali kudanganyika na mjiheshimu.

“Kataeni vishawishi,Mseme hapana kwenye vishawishi na hapana maana yake hapana, epuka marafiki wabaya,vitu vizuri huwa vinachukua muda msiwe na papara na kikubwa mlinde ndoto zenu msizipoteze,”amesema.

Pia ametoa rai kwa vyuo,shule wawe na madawati ya jinsia ili wale wanaofanyiwa vitendo vya kikatili waweze kutoa taarifa.

“Niwaombe katika vyuo na shule kuwajengea uwezo hawa vijana  ili kukabiliana na hizi changamoto,pia mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali na Taasisi mbalimbali tuendelee kulilinda na kulisaidia kundi hili na kikubwa tuwekeze kwenye uwekezaji kiuchumi,”amesema.

Kwa upande wake,Mnufaika wa miradi hiyo,Mariamu Mathias ameiomba Serikali iwasaidie  vikundi vya wasichana balehe na wanawake vijana waweze kupewa kipaumbele katika mikopo inayotolewa katika Halmashauri.
“Ombi letu itusaidie vikundi vyetu vipewe kipaumbele Cha mikopo ya 4-4-2 katika Halmashauri,Serikali itutafutie wadau,”amesema.

Vilevile amesema wameendelea kubaki salama sababu ya kupata elimu ya VVU pamoja na matumizi sahihi ya kondomu.

“Pia  wanapata fursa ya kusomea vitu mbalimbali mfano umeme wa magari,saloon,upishi.Mimi ni mfano halisi wa kusoma masomo hayo na mimi nimesoma Saloon na nimepewa vifaa wezeshi.Nimefanikiwa kupata ajira katika Shirika la Tumaini na ninawasaidia mabinti wenzangu na ninalipwa mshahara wa 650,000.

“Mimi pia nasomesha mdogo wangu na nalea familia yangu na najivunia kuwa kioo kwa mabinti wengine.Sasa hivi sipo katika uhatarishi wa kupata VVU,”amesema.

Naye,Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dk.Leonard Maboko amesema kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2017 unaonesha maambukizi mapya ya VVU asilimia 40 ni vijana wenye umri wa miaka 15-24 huku asilimia 80 wakiwa ni wasichana balehe na wanawake vijana.

“Kwa lugha rahisi katika watu 10 basi wanne ni vijana,tusipochukua tahadhari tutaendelea kuzalisha maambukizi mapya.Ukichukua kundi la vijana ile asilimia 40 basi asilimia 80 ni wanawake,sasa tusiboziba ufa tutajenga ukuta”amesema.

Alisema kuna miradi mikubwa mitatu ambayo inatekelezwa ambayo  ni timiza malengo,Drems,Vijana salama ambapo amedai jumla ya Mikoa 13 imefikiwa na miradi hiyo.

“Jumla ya Mikoa 13 ndio ambayo inapata katika Mikoa 16 na sio katika Halmashauri zote zinakuwa zinachukuliwa,”amesema.

Alisema anatamani kuona vijana wengi wakipata mikopo ili waweze kutimiza ndoto zao ikiwa ni pamoja na kwenye Mikoa ambayo haijafika miradi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles