26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Wasichana wasaidiwa kupata haki ya elimu

Na Mwandishi Wetu -Mara
WADAU mbalimbali nchini wameendelea kutoa msaada wa kielimu kwa familia iliyoshindwa kuwapeleka watoto shule kutokana na hali duni ya maisha waliyokuwa nayo.

Akizungumzia tukio hilo juzi, Msaidizi wa Kisheria Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Anthony Mayunga, alisema kuwa Shirika la Lengo Services Facility limekuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha Watanzania hususani wasioweza kumudu gharama za wanasheria, kupata huduma za kisheria na kutoa msaada katika matatizo mbalimbali ikiwamo mirathi, ndoa, mimba za utotoni, kutelekezwa kwa watoto na ardhi.

Mayunga alisema kuwa hatua hiyo iliwafanya wachukue hatua ya kuhakikisha inawasaidia wanafunzi wawili Magdallena Julius (14) na mdogo wake Hellena Julius (12) ambao wazazi wao walishindwa kuwapatia haki yao ya msingi ya elimu kutokana na hali duni ya maisha wanayokabiliana nayo.

Alisema kuwa kilio hiki kiliwafikia wasaidizi wa kisheria wilayani Serengeti ambao waliamua kuhamasisha jamii, kupitia vyombo vya habari, kuchangia hawa watoto ili wapate haki yao ya elimu. 

“Watoto hawa walihitaji Sh 500,000 kwa ajili ya mahitaji ya shule ikiwemo matengenezo ya viti, meza, michango ya mahindi, sukari, sare na vitu vingine vidogo vidogo vya msingi.

“Kutokana na ushiriki wa vyombo vya habari, watu wengi waliguswa na habari ya watoto hawa na kujitolea kuwasaidia. 

“Mnamo Machi 15 mwaka 2019, Magdallena na mdogo wake, Hellena walionekana wakiwa wenye furaha baada ya kuungana na wanafunzi wenzao wa kidato cha kwanza Serengeti Sekondari na kuanza safari ya kutimiza ndoto zao za kuwa walimu,” alisema Mayunga. 

Shirika la Lengo Services Facility limekuwa mstari wa mbele katika kuwawezesha Watanzania hususani wasioweza kumudu gharama za wanasheria kupata huduma mbalimbali na kufanikiwa. 

Kupitia kwa watoa huduma zaidi ya 3,000 katika kila wilaya Tanzania Bara na Zanzibar, zaidi ya Watanzania milioni tano hufikiwa na kupatiwa elimu ya kisheria na takribani kesi 75,000 zikiripotiwa kwa watoa huduma hao kila mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles