26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 29, 2023

Contact us: [email protected]

Wasichana 300 waokolewa ukeketaji

Na Amina Omari – Kilindi

ZAIDI ya wasichana 300 katika Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga, wameokolewa kufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwamo ukeketaji kutokana na jamii kupata elimu inayotolewa na Shirika la Amref kwa miaka mitano.

Meneja wa Shirika hilo Wilaya ya Kilindi, Jane Sempeho alisema kuanzia Juni, 2014 hadi Desemba mwaka jana,  wasichana 3,786 waliokuwa wafanyiwe ukeketaji waliokolewa na kadhia hiyo.

Alisema shirika hilo limefikia shule 58 za msingi na sekondari na kutoa elimu ya athari za ukeketaji kwa waelimisha rika 348 wakiwemo wahudumu wa afya katika jamii 88.

Sempeho alisema elimu hiyo imejenga ujasiri katika makundi hayo na kuwa walinzi kwa watoto.

Alisema waelimisha rika na wahudumu wa afya katika jamii, wamesaidia kwa kiwango kikubwa kuchangia kuenea kwa elimu na kuleta mabadiliko katika familia zinazoenzi mila hiyo.

Sempeho alisema elimu hiyo inatolewa kwa njia ya mikutano ya hadhara kuelimisha jamii na makundi maalumu ambao ndio mabalozi.

Alisema changamoto wanazokabiliana nazo ni uwepo wa aina tofauti za ukeketaji baina ya kabila moja na jingine, huku kila upande ukiamini hauna madhara.

Sempeho alisema jambo hilo limekuwa likileta ugumu wa mabadiliko haraka kwenye jamii.

Aliwataka wakazi wa wilaya hiyo kuacha mila potofu ikiwemo ya ukeketaji ambayo imeonekana kuwa hatari zaidi kwa wasichana kwa kusababisha madhara ya muda mfupi na yale ya muda mrefu.

Alitaja madhara ya muda mfupi kuwa ni maumivu na hatimaye kupoteza hata fahamu kwa kutokwa na damu nyingi, kupata makovu na maambukizi yamagonjwa, athari wakati wa kujifungua na kumfanya binti kukosa hamu ya tendo la ndoa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles