Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Wateja 100 wa kwanza wa kampeni ya NMB MastaBata-Kivyako Vyako walipatikana jana nakuzawadiwa pesa taslimu Sh 100,000 kila mmoja nataasisi hiyo kiongozi wa shughuli za kifedha nchini.
Washindi hao wamezawadiwa jumla ya Sh milioni 10.
Promosheni ya MastaBata Kivyako Vyako ilizinduliwarasmi katikati ya Desemba mwaka jana ikiwa na lengo la kuchagiza matumizi ya kadi za malipo za Mastercard kama sehemu ya mchango wa NMB katika juhudi zataifa za kujenga uchumi usiotegemea sana fedhataslimu.
NMB pia inatumia kampeni hii ya kuendeleza uchumi wakidijitali kurudisha fadhila kwa wateja wake waaminifuambao wamekuwa ni muhili muhimu wa safari yake yamabadiliko ya kidijitali.
Akizungumza wakati wa droo ya kuwapata washindi wakwanza wa MastaBata-Kivyako Vyako, MenejaMwandamizi wa Wateja Binafsi wa NMB, Ali Ngingite, alisema zaidi ya Sh milioni 200 zitanyakuliwakwenye kampeni hii ya miezi mitatu.
“Hili ni toleo la tatu la kampeni za MastaBata zilizoanzarasmi mwaka 2018 kuwahamasisha wateja na wasiowateja wa Benki ya NMB kutumia kadi za Mastercardwanapofanya malipo na miamala kupitia intaneti.
“Kama watangulizi wake, promosheni ya MastaBata-Kivyako Vyako pia ina lengo la kuwatambua nakuwazawadia wateja wetu waaminifu kwa kuendeleakutumia huduma zetu,” alisema Ngingite ambaye ni mtaalumu wa mikopo binafsi nakuongeza kuwa kutakuwa na droo za kila mwezi naile kubwa ya mwisho.
Wakati washindi 100 wa kila wiki watashinda Sh 100,000 kila mmoja, 25 watanyakua Sh 1,000,000 kilamwezi na 30 wa mwisho watashinda jumla ya Sh milioni 90 zikiwa ni Sh milioni kwa kila mshindi.