30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wasanii wa kike waliopigania uhuru kusakwa

Demere-Kitunga-1NA JONAS MUSHI

MGAHAWA wa Vitabu-Soma umeanza kufanya utafiti wa kuwatambua wasanii wa kike waliosahaulika licha ya kushiriki katika harakati za kupigania uhuru wa Tanzania.

Akizungumza mwishoni mwa wiki katika hafla ya kuwakumbuka wanawake walioshiriki kupigania uhuru, Mkurugenzi wa Soma, Demere Kitunga, alisema wapo wanawake wengi waliopigania uhuru kwa njia ya nyimbo na ushairi lakini wamesahaulika, hawajawekwa hata kwenye vitabu vya historia ya ukombozi.

“Ushiriki wa wanawake kwenye harakati za kupigania uhuru ni mkubwa kuliko inavyojulikana, wengi wanamfahamu Bibi Titi Mohamed, lakini wapo wanawake waliokuwa wakiimba na kutunga mashairi yaliyowatia ari viongozi katika kudai uhuru hawajulikani.

“Tunafanya utafiti kuwapata ambao bado wapo hai ili tupate majina na kazi zao na wale waliofariki tutaweka majina yao katika vitabu vya historia ili mchango wao uweze kuonekana.”

Mtafiti wa Soma, Janet Gabone, alisema changamoto wanayopata ni kutokuwepo mahojiano ya mashuhuda kutambua watu hao kwa kuwa wengi wao hawajaacha kazi zao.

Naye Balozi wa Ireland nchini, Fionnuala Gilsenan, aliwataka wasanii wa Tanzania waongeze bidii katika harakati zao za kupigania mambo mbalimbali katika jamii kwa kuwa nafasi yao ni kubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles