30.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, August 9, 2022

Wasanii kupamba miaka 20 ya Nyerere

BRIGHITER-MASAKI

WASANII wa tasnia mbalimbali nchini, wanatarajia kunogesha sherehe za kumbukumbu ya miaka 20 ya Mwalimu Julius Nyerere zinazotarajia kufanyika leo jijini Dar es salaam.

Takika tamasha hilo, wasanii wanatarajia kutoa tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli pamoja na tuzo ya heshima kwa Mama Maria Nyerere.

Akizungumza na waandishi wa habari msanii Hamisi Mwinjuma maarufu kwa jina la Mwana FA, alisema lazima wasanii wakae pamoja na kukumbuka mchango wa Mwalimu katika kipindi chake, hivyo watakuwa wanahakikisha kila mwaka wanashirikiana kumkumbuka.

“Tamasha la miaka 20 ya Mwalimu litakuwa likifanyika kila mwaka na huu ndio mwanzo, tunataka kulifanya kuwa la kitofauti kwa kuwa haiwezekani watu wa Afrika Kusini waone mchango wa mwalimu na sisi tusione,” alisema Mwana FA.

Kwa upande mwingine msanii Mrisho Mpoto (Mjomba), alisema ingependeza kuwa leo iwe siku ya kutembea peku ikiwa ni ishara ya kumkumbuka mwalimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,291FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles