Wasafi kutafuta wasanii chipukizi

0
912

Brighiter Masaki – Dar es Salaam

WASAFI Media wamezindua michuano ya soka ya Kivumbi Cup itakayoshirikisha timu 32 za mitaani ikiwa pamoja na kusaka vipaji vya wasanii chipukizi wa muziki.

Michuano hiyo itaanza kutimua vumbi Machi 7, ambapo katika kila mchezo kutakuwa na jukwaa la kutafuta wasanii wenye vipaji ambao wanaweza kujiunga na lebo ya WCB.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Meneja wa Diamond Platnumz, Said Fella alisema mashindano hayo ya Kivumbi Cup, yataambatana na mashindano ya kutafuta vipaji kwa waimbaji chipukizi wa muziki wa bongo fleva.

“Temeke ina watu wengi, kutakuwa na waimbaji wa lebo ya Wasafi wakiangalia vipaji vya wasanii chipukizi ili kuona uwezekano wa washindi kusajiliwa kwenye lebo yetu, tunategemea kupata wasanii kupitia michuano hiyo,” alisema Fella

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here