23.6 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 27, 2023

Contact us: [email protected]

WAREMBO VYUO VIKUU JUKWAANI SEPTEMBA 29

Na ESTHER GEORGE-DAR ES SALAAM

WAREMBO wa vyuo vikuu vya Tanzania wanatarajiwa kupanda jukwaani  Septemba  29, mwaka huu kuwania taji la ‘Miss Higher Learning Institution 2017’ kwenye Ukumbi wa King Solomoni, Dar es Salaam.

Mashindano hayo yameandaliwa na Kampuni ya Glamour Bridal Tanzania, baada ya kupewa idhini na waandaaji wa Miss Tanzania, Lino International Agency kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (Basata).

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Glamour Bridal Tanzania, Muba Saedo, alisema wanatarajia kufanya mashindano yenye upinzani wa hali ya juu kutokana na idadi ya vyuo.

Saedo alivitaja vyuo vitakavyoshiriki mashindano hayo ni Taasisi ya Ustawi wa Jamii (ISW), Taasisi ya Uhasibu Dar es Salaam (TIA), IFM, CBE, UDOM, Tumaini–Makumira, Taasisi ya Uhasibu wa Arusha (IAA) na Chuo Kikuu Cha Ardhi.

Vyuo vingine ni Mzumbe, Chuo Kikuu cha Iringa, Tanzania Aviation University College na Magogoni.

Alisema bado wanapokea maombi kutoka vyuo mbalimbali na mwisho wa kuthibitisha ni Septemba 11, mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,729FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles