26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Warembo 15 kuchuana Miss Simiyu

Derick Milton, Simiyu

Shindano la kumtafuta mrembo wa mkoa wa Simiyu ‘Miss Simiyu’ linalo tarajiwa kufanyika Julai 6, mwaka huu litashirikisha jumla ya warembo 15 kutoka mkoani humo.

Shindano hilo ambalo litafanyikia katika uwanja wa halmashauri ya mji wa Bariadi, Mgeni rasmi atakuwa Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson.

Akiongea na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi wa Simiyu Talent Company, Zena Mchujuko ambao ndiyo waandaaji wa shindano hIlo amesema kuwa Miss Simiyu mwaka huu itakuwa kubwa.

Mchujuko amesema kuwa kwa kushirikiana na Grace Entertainment wameamua kuifanya Miss Simiyu kuwa ya kipekee zaidi lengo likiwa mrembo atakayepatikana afike ngazi ya kitaifa hadi dunia.

“ Tutakuwa na mwanamuziki kizazi kipya Diamond Platinumz, ambaye atatoa burudani wakati wa shindano na mgeni rasmi atakuwa Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson,” amesema.

Mchujuko amesema kuwa tiketi zimeanza kupatikana katika maeneo mbalimbali ya mji wa Bariadi, ambapo kiingilio cha chini ni 10,000, 50,000 na VIP 100,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles