27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Wapinzani wasema bado kuna changamoto ya maji

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

KAMBI rasmi ya upinzani bungeni imesema kuna ushahidi wa kutosha kuwa ndoa nyingi zimevunjika kutokana na changamoto za maji, hivyo inatosha kusema kampeni ya kumtua mwanamke ndoo kichwani imeshindwa.

Akiwasilisha maoni ya kambi hiyo msemaji  wa Wizara ya Maji  kwa upinzani, Zubeda Sakuru alisema wanawake ndio wamekuwa wahathirika wakubwa kwa matukio ya udhalilishaji na ukatili kama vile ubakaji na kesi nyingine nyingi za kudhuru mwili wanazokumbana nazo wakiwa katika safari za kutafuta maji.

Alisema kuna ushahidi wa kutosha kuwa ndoa nyingi zimevunjika kutokana na changamoto za maji, hivyo inatosha kusema kampeni ya kumtua mwanamke ndoo kichwani imeshindwa.

“Ili kukabiliana na changamoto za kimazingira na kiafya zinatojitokeza kwa kushindwa kuwa na mifumo hiyo hasa katika kipindi hichi cha mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanawake wanapata maji,” alisema Sakuru. 

Alisema Kambi ya Upinzani inaitaka Serikali kutoweka mazingira ya usiri na ubabaishaji katika kutekeleza miradi ambayo inalenga kuwapa wananchi maji safi na salama.

“Serikali kujitafakari kwa kina ni kwa kiwango gani imeweza kutatua changamoto za maji nchini hasa kwa kuhakikisha kuwa Watanzania wanapata maji safi na salama.

“Lakini kwa kuwataka waheshimiwa wabunge hasa ambao walitumia tatizo la uhaba wa maji katika majimbo yao kama kete ya kuombea kura kwa wananchi, je, ndani ya miaka mitano ya awamu ya tano wameweza kutatua kero ya maji katika majimbo yao?” alihoji Sakuru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles