25.1 C
Dar es Salaam
Saturday, December 9, 2023

Contact us: [email protected]

Wapinzani Uganda wafurahi Besigye, Bobi Wine kukutana

KAMPALA, UGANDA

CHAMA cha upinzani  cha Democratic Party (DP) kimeeleza kwamba kitendo cha Rais wa zamani wa Chama cha Forum for Democratic Change (FDC), Dk. Kizza Besigye na Mbunge wa Jimbo la  Kyadondo Mashariki, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine kukutana ni hatua moja nzuri ya kujenga umoja ndani ya upinzani.

Kauli ya chama hicho imekuja baada ya kuwapo lawama kutoka kwa baadhi ya wanasiasa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa kuhusu kitendo cha wanasiasa hao maarufu kukutana.

Hata hivyo, Msemaji wa DP, Kenneth Kakande alisema kwamba kikao hicho ni ishara nzuri ambayo inapaswa kuzingatiwa.

 “Tumefurahia hatua ya Besigye na Kyagulanyi kukutana. Hii inaonesha kwamba tunaweza kufanya kazi kwa pamoja kama watu wapenda mabadiliko,” alisema.

Kakande ambaye alikuwa akizungumza na waandishi wa habari juzi katika kikao chake cha kila wiki makao makuu ya chama hicho, alisema kuwa wapinzani wanaweza kupiga hatua kubwa endapo watakuwa wakifanya kazi kwa pamoja.

“Endapo tutajenga umoja wetu tunaweza kufikia kile ambacho tunakitaka. Tunataka kuwa na mgombea mmoja wa urais na nafasi sawa katika uchaguzi wa ngazi za chini. Hii itatusaidia kutogawanya kura,” alisema Kakande.

Msemaji huyo alielezea wasiwasi wake hatua ya hivi karibuni ya kuweka vikosi vya ulinzi wa mitaa (LDU), akisema kuwa umma umekuwa ukilalamika kubambikiwa kesi kuharibu mali zao na kuwatesa.

Hata hivyo katika mahojaino na gazeti la New Vision, Msemaji wa Polisi, Fred Enanga, alisema kwamba watashirikiana na vikosi vya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi (UPDF) kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo.

Enanga aliwataka wananchi mara zote kutoa taarifa za askari hao wa LDU katika vituo vyao vilivyopo karibu, na akafafanua kuwa askari hao wapo chini ya UPDF, lakini wanasimamiwa na polisi kutegemeana na maeneo walikopelekwa na akafafanua kuwa hadi sasa hajapokea malalamiko yoyote kutoka kwa wananchi kuhusu vitendo viovu vinavyofanywa na askari hao.

Kwa mujibu wa gazeti la New Vision, takribani askari  6,000  wa LDU walipewa mafunzo ili kuliongeza nguvu Jeshi la Polisi ili kukabiliana na uhalifu mjini hapa na maeneo ya jirani ya Wakiso na Mukono.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles