25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Wapigwa faini mil 700/- kwa uvuvi haramu

MWANDISHI MAALUM-MTWARA

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa Kanda ya Mtwara, imewahukumu watu watatu wakiwamo raia wawili wa kigeni na Mtanzania mmoja kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja au kulipa faini ya Sh bilioni 1 baada ya kukamatwa wakifanya uvuvi haramu katika Ukanda wa Bahari Kuu Januari mwaka huu.

Watu hao walikamatwa katika ‘Operesheni NMATT’ iliyokuwa inaendeshwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola katika Meli ya Buah Naga 1 ya nchini Malaysia wakiwa na kilo 90 za mapezi ya papa bila kuwa na miili yake kinyume cha Sheria kati ya  mikoa ya Lindi na Mtwara na kutakiwa kulipa faini ya Sh milioni 770 ambapo walikwenda mahakamani kupinga adhabu hiyo.

Akisoma hukumu hiyo mwishoni mwa wiki, Jaji wa Mahakama  Kuu Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Makosa ya Rushwa Kanda ya Mtwara, Lilian Mashaka alisema washtakiwa hao walikiri kutenda kosa hilo ambapo kwa mujibu wa kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi Namba 2 ya mwaka 2018, Mahakama imewakuta na hatia na kutoa adhabu hiyo.

Jaji Mashaka aliwataja washtakiwa kuwa ni pamoja na Nahodha wa meli hiyo,  Han Ming Chuan, Raia wa China, Mmiliki wa Meli hiyo, Dato Seri Lee Raia wa Malaysia na Wakala wa Meli hiyo, Abubakar Salum,  Raia wa Tanzania.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,407FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles