25.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wapiga kura Ugiriki kumng’oa Tsipras

BRUSSELS-UGIRIKI

RAIA wa Ugiriki jana walipiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa Taifa hilo tangu kumalizika enzi ya mpango wa kuokoa uchumi wa nchi hiyo.

Ubelgiji ni miongoni mwa mataifa yaliyoanza mwanzo baada ya mdodoro wa uchumi kuikumba dunia miaka michache iliyopita.

Katika uchaguzi huo wa kwanza baada ya nchi hiyo kuokolewa kiuchumi chama cha Waziri Mkuu, Alexis Tsipras cha mrengo wa kushoto cha Syriza kinatarajiwa kung’atuliwa madarakani na chama cha upinzani cha kihafidhina ambacho kimeonekana wazi kuleta ushawishi mkubwa.

Baada ya takriban miaka mitano mamlakani, waziri huyo mkuu wa Ugiriki, anang’ang’ania kuziba nakisi ya pointi 10 katika kura ya maoni huku umaarufu wake ukipungua kote nchini baada ya miaka mingi ya kodi kubwa.

Vituo vya kupiga kura vilifunguliwa jana saa moja asubuhi na vilitarajia kufugwa jana saa moja usiku.

Kwa mujibu wa Shirika la habari la Athens, raia takriban milioni 10 walijiandikisha kupiga kura.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles