25.7 C
Dar es Salaam
Saturday, December 4, 2021

Wapandishwa kizimbani kwa ubakaji

AVELINE KITOMARY-DAR ES SALAAM 

MKAZI wa Sinza “E”, John Julius (33) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni  Dar es Salaam   akituhumiwa kwa   ubakaji.

Akisoma shtaka hilo mbele ya Hakimu Bonifasi Lihamwike, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Veronika Mtafia, alidai   kuwa  Januari 26 mwaka huu eneo la Sinza kwa Remy Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam, mshtakiwa alimwingilia na kumbaka bila idhini yake, Ester Michael (32).  

Mshtakiwa alikana mashitaka na Hakimu Lihamwike alisema dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili  watakaotoa bondi ya Sh milioni moja.

Hata hivyo mshatakiwa alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kurudishwa rumande mpaka kesi yake itakapotajwa  tena Feburuari 28 mwaka huu.

Wakati huo huo, mkazi wa Goba wilayani Ubungo mkoa wa Dar eSalaam, Richard Mhimbira (35)  amepandishwa kizimbani kwa shtaka la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. 

Akisoma shtaka mbele ya Hakimu, Joyce Mushi, Wakili wa Serikali, Grace Lwila alidai kati ya Agosti 8 na Oktoba 5,2018 eneo la Mlimani City, Wilaya ya Kinondoni, mtuhumiwa alijipatia  Sh15,751,957 kutoka kwa Gibonce Kajigili  kwa akidai kumuuzia gari kitu ambacho hakikuwa kweli.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na alirudishwa rumande   hadi  Februari 27 mwaka huu kesi yake itakapotajwa  tena.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,875FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles