24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Waomba kusaidiwa viti mwendo, bima ya afya

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Baadhi ya wazazi wenye watoto wenye ulemavu wanaosoma katika Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko wamewaomba wadau kujitokeza kuwasaidia viti mwendo na bima ya afya ili watoto wao waweze kusoma katika mazingira mazuri.

Zulfa Abdallah akiwa na mwanawe Nuru Isihaka mwenye ulemavu wa akili na viungo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti shuleni hapo Zulfa Abdallah mzazi wa Nuru Isihaka (6) mwenye ulemavu wa viungo na akili amesema kila siku analazimika kumbeba mwanawe mgongoni pindi anapompeleka shule na kumrudisha.

“Mwanangu hawezi kutembea huwa anatambaa tu chini kwahiyo asubuhi lazima nimbebe mgongoni kumleta shule na mchana ninapokuja kumchukua. Naomba wasamaria wema wanisaidie mwanangu aweze kupata baiskeli ya kutembelea (kiti mwendo),” amesema Zulfa.

Naye Angelina Cyrpian mzazi wa Ibrahim Said (9) mwenye ulemavu wa akili na viungo ameomba wasamaria wema wamsaidie mwanawe aweze kupata bima ya afya.

Angelina ambaye ni mkazi wa Buguruni Kisiwani amesema hana shughuli yoyote ya kumuingizia kipato na kwamba wazazi wake ndiyo wanaomsaidia katika matunzo ya mwanawe.

Mzazi mwingine Fatuma Katundu ambaye ni mlezi wa Shadya Ramadhani (10) mwenye ulemavu wa akili, ameomba asaidiwe bima ya afya kwani mjukuu wake amekuwa akitumia dawa kila siku kutokana na matatizo aliyonayo.

“Kila siku anameza dawa na huwa nanunua za siku 10, kwahiyo nikipata bima ya afya itasaidia nitakuwa nachukua hata za mwezi mzima,” amesema Fatuma.

Aidha amesema mjukuu wake alitelekezwa na mama yake mzazi tangu akiwa na miaka miwili na toka wakati huo hawajawahi kumuona.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko, Christina Wambura, amesema shule hiyo ina wanafunzi 114 wenye ulemavu wa aina mbalimbali. Wanafunzi wenye ulemavu na idadi yao kwenye mabano ni wasioona (47), viziwi wasioona (10) na ulemavu wa akili (57) ambao wakekuwa wakifanya vizuri kitaaluma.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles