27.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 7, 2023

Contact us: [email protected]

WAOMBA ENEO KUCHIMBA ALMASI

WACHIMBAJI wadogo wa almasi wilayani  Kishapu, maarufu kwa jina la Wabeshi, wamemuomba Rais John Magufuli kuwasaidia kutengewa eneo la kuchimba madini hayo, anaripoti Kadama Malunde.

Kwa mujibu wa wachimbaji hao, hatua hiyo itawasaidia kupunguza uvamizi wa Mgodi wa Almasi wa Williamson.

 Wakizunguza na waandishi wa habari hivi karibuni kwa nyakati tofauti, Wabeshi hao walisema vijana wengi wakazi wa maeneo yanayozunguka mgodi huo wamekuwa wakitafuta namna ya kujiajiri.

  Mabula Njile mkazi wa kijiji cha Nyenze Kata ya Mwadui Luhumbo, alisema endapo serikali itawapatia maeneo kwa ajili yao sehemu kubwa ya vijana hao hawataendeela na uvamizi mgodi wa Williamson.

  Juma Ng’ombeyapi kutoka Kijiji cha Ng’wang’holo, alisema hajawahi kuona kiongozi yeyote wa juu wa serikali akifika katika maeneo yanayozunguka mgodi huo   kusikiliza kero za wananchi.

 Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Talaba alionyeshwa kushangazwa na madai ya wachimbaji hao ambao alisema  tayari walishapewa maeneo ya kuchimba lakini hawataki kuyaendeleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,885FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles