Na Mwandishi Wetu
JUMLA ya waogeleaji 14 wameunda timu ya Taifa kujiandaa na mashindano ya vijana ya kuogelea ya Afrika yatakayofanyika kuanzia April 30, hadi Mei 3, mwaka huu nchini Misri.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Chama cha Kuogelea Tanzania (TSA), Sebastian Kolowa timu hiyo imeshaanza maandalizi ya michuano hiyo kuhakikisha inakwenda kushiriki na kufanya vizuri.
“Kati ya waogeleaji hao, saba ni wanaume na wengine saba ni wanawake. Uchaguzi wa kikosi umetokana na mashindano mbalimbali yaliyopita ikiwemo iliyofanyika wiki mbili zilizopita,”amesema.
Waogeleaji hao ni Romeo Mwaipasi, Aryan Bhatt, Mark Tibazarwa, Austin Okore, Christian Fernandes, Enrico Baretto, Sahal Haarunani.
Wengine ni Filbertha Demello, Lina Goyayi, Bridget Heep, Natalia Ladha, Amylia Chali, Aliyana Kachra na Aminaz Kachra.