29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WANYWA POMBE ZA VIROBA WABUNI MBINU MPYA

Na RAMADHAN HASSAN -DODOMA


WANYWAJI wa pombe za viroba mjini Dodoma wamebuni mbinu mpya ya kununua pombe hiyo iliyopigwa marufuku.

Wakati wa kununua pombe hiyo, watumiaji hao wameipa jina la maziwa mgando au nzela.

Miongoni mwa maeneo yanakopatikana viroba kwa wingi mjini hapa ni Jamatini na stendi ya Mkoa wa Dodoma, ambako wafanyabiashara humimina pombe hiyo katika chupa za konyagi.

Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA kwa siku kadhaa mjini hapa, umeonyesha jinsi pombe hiyo inavyouzwa kwa Sh 1,000 baada ya kujazwa kwenye chupa kubwa za konyaji.

Mmoja wa wauzaji wa pombe hiyo ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini, alisema biashara imekuwa ngumu na wao wanahitaji kupata fedha, hivyo wameamua kuja na njia mpya ya kuuza viroba hivyo.

“Tutafanyaje ndugu yangu, maisha magumu, tumeweka viroba katika chupa kubwa za konyagi na tunawapimia kwa kutumia kakikombe kadogo kama ka kahawa kwa shilingi 1,000,’’ alisema mfanyabiashara huyo.

“Siwezi kuacha hii biashara, hapa ni stendi, wasafiri na makondakta wengi ndio wateja wetu na natengeneza fedha za kutosha, lakini sasa hivi nawauzia tu watu ninaowajua, kwani naogopa kukamatwa,” alisema.

Naye mmoja wa wanunuzi wa viroba hivyo, alisema baada ya Serikali kupiga marufuku uuzwaji wa viroba hivyo, wameamua kubadili mwelekeo wa kununua bidhaa hiyo ili kukwepa mkono wa Serikali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles