25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

WANYAMA WALIOWAHI KUSHINDA NYADHIFA KWENYE UCHAGUZI

NA JOSEPH HIZA,

SHERIA ZA uchaguzi kwa kawaida huhitaji wagombea wanadamu au kuwakilishwa kwa vivuli vyao iwe picha au majina yao.

Lakini imetokea katika baadhi ya nchi duniani uwapo wa wagombea wasio wanadamu hasa wakitumika wanyama kuwania nyadhifa au kufanya kazi za kibinadamu.

Mara nyingi wagombea hawa hutumika kama kura ya kupinga jambo au mgombea fulani au kuukejeli, kura ya hasira ama kubeza mfumo wa kisiasa.

Wakati mwingine uchaguzi wa wanyama hufanyika kwa malengo ya kujifurahisha.

Linapokuja kwa wanyama hawa kuchukua nafasi ya binadamu kuwania nyadhifa, binadamu huchukua nafasi ya kile ambacho mnyama huenda asiweze kukifanya kama vile kusaini majina yao katika fomu.

Katika badhi ya matukio, wanyama wamekubalika kama wagombea na kushinda chaguzi.

Wafuatao ni wanyama waliowahi kushinda chaguzi. 

Mbwa meya

Mbwa aliyeenda kwa jina Duke alichaguliwa kwa mara ya tatu kuwa meya wa mji wa Cormorant jimbo la Minnesota, Marekani.

Kuna Junior Cochran, mbwa mweusi aina ya Labrador, aliyechaguliwa kuwa meya mji wa Rabbit Hash, Kentucky, pia nchini humo mwaka 2004.

Aidha, huwezi kumsahau Bosco mbwa aliyehudumu kama meya wa Sunol, California, kuanzia 1981 hadi 1994 kiasi cha kuwepo sanamu ya ukumbusho wake.

a aliyejulikana kama Bosco

Paka waliochaguliwa kuwa mameya

Paka aliyejulikana kwa jina la Stubbs alichaguliwa meya wa Talkeetna, Alaska nchini Marekani mwaka 1997.

Kuna akaunti ya Twitter yenye jina lake ikiwa na maelezo: “Mimi ni paka. Nilichaguliwa Meya wa Alaska. Karibuni, nitakuwa rais.”

kwa jina Stubbs

 Kifaru aliyechaguliwa kuongoza Sao Paulo

Mwaka 1959, kifaru wa umri wa miaka mitano kwa jina Cacareco alichaguliwa meya wa mji wa Sao Paulo nchini Brazil kwa kura nyingi.

Cacareco, jina ambalo maana yake ni ‘taka’ kwa Kireno, aliandikishwa kwenye kura kama hatua ya kulalamikia ufisadi miongoni mwa wanasiasa.

Hakuchukua mamlaka hata hivyo kwani uchaguzi ulirudiwa.

Mbuzi kiongozi wa New Zealand

Iwapo bado umeshangaa, tulia, eneo la Whangamomona nchini New Zealand, mbuzi aitwaye Billy Gumboot mwaka 1999 alichaguliwa kuwa rais.

Alikuwa mnyama wa kwanza kuchaguliwa katika wilaya hiyo lakini hakuwa wa mwisho, baada yake kuondoka madarakani, mrithi wake alikuwa mbwa aina ya Poodle aliyepewa jina Tai.

Kwa sasa eneo hilo linaongozwa na rais wa kwanza mwanamke, Vicki Pratt.

Sokwe wa Rio de Janeiro

Sokwe kwa jina Tiao alipata kura nyingi, ingawa hazikutosha kabisa kumfanya meya wa mji wa Rio de Janeiro. Kauli mbiu yake ilikuwa: “Mpigie kura tumbili – upate tumbili.” Lakini alienziwa kwa sanamu.

Brigedia Pengwini

Ndege mnene wa majini Pengwini aliyepwa jina la Nils Olav alipewa cheo cha Brigedia katika jeshi la Norway, na hata akakubaliwa kutekeleza majukumu rasmi, ikiwamo kukwagua ua gwaride.

 Paka kiongozi wa chama cha kisiasa Uingereza

Paka anayeitwa Mandu nchini Uingereza, alihudumu kama kiongozi mwenza wa chama cha Official Monster Raving Loony Party kuanzia 1999 hadi 2002.

Ndiye paka pekee aliyewahi kuongoza chama cha kisiasa.

Tovuti ya chama hicho inasema: “Kilikuwa kinyang’anyiro kikali kati ya Howling ‘Laud’ Hope na Paka Mandu.

“Walikaribiana sana kwa kura. Wote walipata kura 112 kila mmoja na ikaamuliwa washikilie wadhifa huo kwa pamoja.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles