31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

‘WANYAMA WA HIFADHI YA SERENGETI NI TATIZO’

go-on-travel-raubkatzen-17-750x500

Na MALIMA  LUBASHA-SERENGETI

SERIKALI imesema  inatambua   na kuzifanyia kazi changamoto  za wanyama mbalimbali wakiwamo Tembo kutoka Hifadhi ya Serengeti kuvamia makazi ya watu na kufanya uharibifu au kujeruhi na hata kusababisha vifo.

Pia imesema migogoro ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)  na tozo za kuingia ndani za  hifadhi hizo zinashughulikiwa kwa haraka ili kupata mwafaka.

Kauli hiyo imetolewa  jana na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani,wakati akizungumza na viongozi wa Wilaya ya Serengeti katika ziara yake ya kikazi ya siku moja wilayani humo.

Makani alikiri  Serikali  kuwa na taarifa ya changamoto hizo kuhusu malalamiko ya wananchi ya tembo kuvamia makazi yao na kula mazao na kusababisha mauaji  ya watu na mifugo  hivyo inafanya kila linalowezekana kutoa kifuta machozi.

“ Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli, imeahidi kutekeleza ahadi zote zinazowakabili wananchi na inapenda wanaoishi jirani na hifadhi kuishi kwa usalama na amani na kunufaika na hifadhi hiyo kwani wao ndio walinzi wa kwanza wa rasilimali zilizomo,”alisema.

Hata hivyo Mwenyekiti wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM), Wilaya ya Serengeti, Vicent Nyamasagi, alisema changamoto nyingine iliyopo ni tozo wanazotozwa watalii wanaoingia ikiwa ni pamoja wananchi kwamba imezorotesha utalii.

Nyamasagi aliomba Serikali kuingilia kati mgogoro wa mpaka wa Hifadhi ya Serengeti na wananchi ambapo Tanapa imeamua kuchukua maeneo ya wananchi bila kuwashirikisha jambo ambalo limeleta migongano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles