32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

WANYAMA ATIWA MZUKA NA SIMBA, YANGA

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

UPINZANI unaoonyeshwa na klabu kongwe nchini, Simba na Yanga, umeonyesha kumvutia mchezaji wa kimataifa wa Kenya, anayechezea klabu ya Tottenham Hotspurs, kiungo mkabaji Victor Wanyama.

Simba na Yanga ni wapinzani wa jadi nchini, ambapo upinzani wao umekuwa ukikua siku hadi siku, hali inayofanya mchezo kati ya timu hizo mbili kuingia katika rekodi ya mapambano bora Afrika.

Ukiacha pambano kati ya timu za Super Sports na Mamelody Sundown za Afrika Kusini, Hearts of Oak na Asante Kotoko ya Ghana, hutaacha kuzungumzia pambalo lingine bora ambalo linakutanisha timu hizi za Simba na Yanga na kuvuta hisia za mashabiki wengi.

Wanyama yupo nchini kwa ajili ya mapumziko, baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu nchini England, ambapo ameambatana na wadogo zake.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Wanyama alisema timu hizo zimekuwa zikimvutia kutokana na upinzani wao unaoleta tija katika soka la Tanzania.

“Atakayekwambia hazijui klabu za Simba na Yanga atakuwa anakosa raha sana, navutiwa na upinzani wao, ambao kwa hakika unalitangaza soka la Tanzania.

“Huwezi kulitaja soka la Tanzania bila kutaja klabu hizo, zinajulikana na nina imani hata baadhi ya watu na timu kubwa barani Ulaya zinasikia kuhusu hizi timu,” alisema Wanyama.

Lakini Wanyama alieleza kuwa, kabla ya kupata nafasi kucheza soka la kulipwa Ulaya, hakuwahi kufikiria kucheza katika klabu hizo, isipokuwa Azam.

“Sikuwahi kufikiria kucheza katika klabu hizo, licha ya umaarufu wake, ila Azam niliwahi kuifikiria na hii ni kutokana na urafiki wangu na Yusuph Bakhresa,” alisema.

MTANZANIA lilimpata Yusuph, ambaye naye alieleza kuwa, kama klabu wangefarijika kama Wanyama angeamua kutua katika klabu hiyo, kwani ni mchezaji mkubwa.

“Ingekuwa faraja kubwa kwetu kama Wanyama angecheza Azam na mafanikio yake angeanzia kuyapata akiwa na timu yetu, hakuna klabu ambayo haitamani kuwa na mchezaji kama yeye, ila tunamkaribisha wakati mwingine akiona inafaa kucheza Azam,” alisema Yusuph.

Akizungumzia soka la Tanzania, Wanyama alisema linazidi kupiga hatua, japo kuna nguvu ya ziada inahitajika kuweza kulisukuma kufikia mafanikio makubwa.

Hata hivyo, mchezaji huyo jana alikuwa mmoja kati ya watu walioshuhudia mchezo wa Ndondo Cup kati ya Kauzu FC na Faru Jeuri, katika Uwanja wa Kinesi, michuano ambayo imekuwa gumzo nchini kutokana na kuibua vipaji.

Kabla ya kushuhudia mchezo huo, Wanyama alisema anavutiwa na michuano ya aina hiyo, kwani inatoa fursa kwa wachezaji kuonyesha uwezo wao, hasa wale wasiokuwa na timu zinazoshiriki Ligi.

Wanyama aliwahi kucheza klabu za Nairobi City Star, AFC Leopards Helsingborg zote za nchini Kenya,

Baada ya hapo, nyota huyo alicheza ligi ya Ubelgiji akiwa na timu ya Beerschot, kabla ya kuhamia Celtic, Southampton na Tottenham, zote za Ligi ya Uingereza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles