25.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wafanyabiashara Pangani watakiwa kuuza sukari bei elekezi

Na Amina Omari – Pangani

WAFANYABIASHARA wilayani Pangani mkoani Tanga wametakiwa kufuata agizo la Serikali la kuuza sukari kwa bei elekezi ya Sh 2,700 na atakayekiuka atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Hayo yalisemwa juzi na Ofisa Biashara wa wilaya hiyo, Mohamed Hussein wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuwaonya wafanyabiashara  kutotumia mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kuwapandishia wananchi bei.

Alisema  kufanya hiyo ni kukiuka sheria na atakayebainika atachukuliwa hatua ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili iwe fundisho kwa wengine.

“Niwatake wafanyabiashara muuze sukari kwa bei iliyopendekezwa na Serikali,” alisema Hussein na kuwasisitiza wananchi kutoa taarifa jeshi la polisi endapo kutakuwa na mfanyabiashara anaekiuka agizo hilo.

Aliwataka wafanyabiashara wafuate sheria bila shuruti kwa sababu Serikali ilishafanya utafiti na kujua bei ya sukari.

“Wasitumie mfungo huu wa Ramadhani kuwabambikia bei wananchi, atakayekiuka maagizo atakumbana na sheria na wananchi wasisite kutoa taarifa jeshi la polisi au halmashuri endapo watauziwa sukari kinyume na bei elekezi,” alisema Hussein.

Alisema kwa wilaya hiyo bado kuna changamoto ya utekelezaji wa agizo hilo kutokana na wafanyabiashara kudai kuwa wamenunua sukari kwa bei ambayo inawalazimu kuuza Sh 3,200 na kusisitiza atakayekiuka agizo la Serikali atapigwa faini.

Katika hatua nyingine, Hussein alisema Serikali imepeleka  sukari takribani tani 22,000 ambazo wafanyabiashara watanunua na kuuza kwa bei elekezi.

Machi 24, mwaka huu, Serikali ilitangaza bei elekezi ya sukari kupitia gazeti la serikali no 284 ambayo kwa Mkoa wa Tanga ni Sh 2,700 kwa kilo moja.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles