24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wanunuzi wa pamba washangazwa mfumo wa malipo kwa wakulima

Na Derick Milton, Simiyu

Wanunuzi wa zao la pamba wameeleza kushangazwa na maamuzi ya serikali katika msimu mpya wa ununuzi wa zao hilo 2021/22 ya kuruhusu malipo ya wakulima wa pamba kufanyika kwa njia ya mkono au pesa taslimu.

Wamesema kuwa maagizo ya serikali kabla ya msimu kuzinduliwa yalitolewa na Mawaziri kwa nyakati tofauti yalikuwa, malipo ya wakulima katika msimu huu yafanyika kwa njia ya benki au mitandao ya simu.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo Jumatano Mei atibu wa Chama cha wanunuzi wa zao hilo nchini (TCA), Boaz Ogolla amesema kuwa wameshangazwa na maamuzi hayo ambayo yanaendelea kuweka mazingira magumu ya pesa zao na wakulima.

Ogolla amesema kuwa wao kama wanunuzi walikuwa wamejipanga kulipa wakulima kwa njia za benki au mitandao ya simu na malipo yangelifanyika kwa haraka lakini mwongozo wa serikali ambao uliletwa iliruhusu malipo ya mkono kufanyika.

“Mwongozo ambao ulikuja umesema malipo yanaweza kufanyika kwa njia ya pesa taslimu, benki au simu, wakulima na Amcos wao ndiyo waamue walipwe kwa njia gani, baada ya kuanza kununua wakulima wote wanataka kulipwa kwa mkono,” amesema Ogolla.

Amesema kuwa baada ya mwongozo wa serikali kutolewa, Amcos nyingi zimeegemea upande wa pesa taslimu, na hakuna amcos ambayo imeomba malipo ya wakulima wake yapitie benki au kwa kutumia mitandao ya simu.

Ogolla ameeleza kuwa pesa kulipwa kwa njia ya taslimu, itasababisha matatizo ambayo yalikuwepo uko nyuma yaweze kujirudia ikiwemo wizi wa pesa za wakulima, ikiwa pamoja na upotevu wa pesa za wanunuzi.

Aidha ameongeza kuwa Amcos nyingi hazina uwezo wa kutunza pesa nyingi, hivyo kusababisha usalama mdogo wa pesa zao kama wanunuzi lakini pia pesa za wakulima ikiwa Amcos itaachiwa pesa nyingi na zikapotea.

“Serikali iliagiza benki kuwafungulia wakulima akaunti na benki nyingi zilifanya hivyo, kwa uamuzi huu hizo akaunti hazitafanya kazi tena hiyo ni hasara kwa benki, lakini usalama wa pesa zetu hautakuwepo,” amesema Ogolla.

Katibu huyo amesema kuwa katika msimu huu wa pamba zaidi ya Sh bilioni 300 zitatolewa kwa wakulima kama malipo ya pamba yao na zitatolewa kwa taslimu, hali ambayo amesema itasababisha serikali kukosa mapato.

Wanunuzi hao wameiomba serikali kusimamia maagizo yake na mfumo wa ulipaji wa wakulima kwa njia ya benki au mitandao ya simu utumike ili kuwepo na usalama wa pesa zao na wakulima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles