23 C
Dar es Salaam
Monday, August 15, 2022

Wanawake wenye matatizo kuombewa dua Diamond

Sheikh Msopa
Sheikh Msopa

Na Yassin Issah-Dar es Salaam

WANAWAKE wenye matatizo mbalimbali ya kiafya, majini na mikosi wataombewa dua bure Septemba 30, mwaka huu katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, kuanzia saa moja asubuhi hadi 12 za jioni.

Dua hiyo itaendeshwa na Sheikh Hussein Msopa, maarufu kama Sharifu Majini, ambaye hufanya shughuli hiyo Mabibo Dar es Salaam, ambapo tukio hilo litaendeshwa bure kwa wanawake wote watakaohudhuria.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Sheikh Msopa alisema lengo la dua hiyo ni kwa ajili ya kuwasaidia akinamama wenye matatizo makubwa, yakiwamo yale yanayohusiana na majini yanayosumbua akinamama wengi hapa nchini.

Alisema mara kadhaa wagonjwa wenye matatizo hayo huwanyima raha watu na wakati mwingine kuzuia riziki na kuwasababishia changamoto nyingi, jambo linalomfanya aiweke siku hiyo iwe maalumu kwa ajili ya kutafuta namna ya kuwasaidia watu hao.

“Nimeipanga Septemba 30, mwaka huu katika ukumbi wa Diamond, iwe siku muhimu kwa ajili ya kutoa elimu ya dua ninazotoa katika ofisi yangu sanjari na kuwasaidia akinamama wenye matatizo yote yakiwamo ya ujauzito kwa sababu ya kuzuiwa na majini, wenye mikosi nikiamini kuwa hatua hiyo itakuwa nzuri kwa watu wote.

“Dua zitaanza saa moja asubuhi hadi 12 jioni na hakutakuwa na kiingilio chochote kwenye tukio hilo ambapo nimedhamiria kiasi kikubwa kuleta furaha na amani kwa akina mama wanaosumbuliwa na matatizo mbalimbali,” alisema Msopa.

Kwa mujibu wa sheikh Sharifu Majini, taarifa za dua hiyo zitaendelea kutolewa kwa njia mbalimbali za mawasiliano ili kutoa fursa ya watu wengi kufahamu na kujumuika pamoja kwenye tukio hilo lenye nia ya kuwasaidia akina mama wanaoendelea kutaabishwa na majini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,800FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles