30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake watakiwa kuzingatia ya wataalamu

MWANDISHI WETU-NJOMBE

WANAWAKE mkoani Njombe wametakiwa kufuata maelekezo na ushauri wa wataalamu wa afya katika malezi na ukuaji wa mtoto kutoka kipindi cha kuzaliwa mpaka anapofikisha umri wa miaka mitano ili kuweza kumsaidia mama na mtoto kuwa na afya njema.  

Hayo yamesemwa na mratibu wa Afya ya Mama na Mtoto wa Wilaya ya Wanging’ombe, Edshan Mtega wakati wa shughuli ya kina mama wenye watoto wa chini ya mwaka mmoja iliyoandaliwa na mradi wa USAID TULONGE AFYA kupitia jukwaa la NAWEZA kwa kushirikiana na uongozi timu ya afya ya wilaya wa Wanging’ombe.  

Akizungumza kwenye shughuli hiyo iliyopewa jina la  “Mothers Meet Up Events” ikimaanisha “Shughuli ya Kukutana kina Mama” ambayo ilifanyika katika ya wilaya ya Wanging’ombe wisho wa wiki hii Mratibu huyo wa Afya ya Mama na Mtoto wilayani Wanging’ombe, Edshan Mtega alilisisitiza kuwa malezi bora kwa mtoto chini ya miezi sita ni muhimu sana katika kuchochea afya njema kwa mtoto katika kipindi cha utotoni mpaka anapokuwa mtu mzima.

Mtega alisema kuwa lengo la shughuli hiyo ni kupeana uzoefu na kukumbushiana kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa malezi ya mtoto kuanzia kipindi cha kuzaliwa mpaka kufikia umri wa miaka mitano ikiwemo Mama kulala na kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama kwa kipindi miezi sita bila kumpa kitu chochote, kulala kwenye chandarua chenye dawa kila siku na matumizi ya njia za kisasa za afya ya uzazi.

“Matumizi ya njia za kisasa za afya ya uzazi ni muhimu kwani inatoa nafasi kwa mama kufanya shughuli zaidi za kiuchumi, mtoto anakuwa vizuri na vile vile wazazi uweza kuamua muda muafaka wa kupata mtoto mwingine,” alisema Mtega.

Mtega aliwasisitiza pia mama anapoona dalili hatarishi kwa mtoto ni vyema akampeleka hospitali kupata matibabu sahihi na kuondokana na Imani potofu na kufikia akina mama wengine kwenda kupata tiba ya miti shamba ambayo inaweza kuhatarisha zaidi Maisha ya mtoto.

Alitoa shukrani kwa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo wilayani humo ikiwamo mradi ya Tulonge Afya unaotekelezwa kupitia ufadhili wa shirika la Marekani liitwalo USAID.  Mradi wa USAID Tulonge Afya unahamasisha mabadiliko ya tabia chanya ndani ya jamii ili kuiwezesha kuwa na Afya njema. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles