27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wanawake watakiwa kujikubali katika uongozi

Na Leonard Mang’oha, Kilimanjaro

Wanawake wametakiwa kujenga tabia ya kujikubali na kujiamini katika masuala mbalimbali hususan yanayohusu uongozi ili kuwa na usawa wa kijinsia katika kuamua masuala mbalimbali ya kijamii na kiuchumi.

Hayo yamebainishwa Alhamisi Oktoba 6, 2022 wakati wa warsha katika tamasha na jinsia la siku linaloendelea wilayani Same Mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumza wakati wa warsha hizo zilizoratibiwa wawakilishi wa taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali zinazoshiriki tamasha hilo, mmoja wa washiriki, Essau Njenda amesema wanawake wanakabiliwa na changamoto ya kukosa mshikamano pale mwanamke wenzao anathubutu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi.

“Wanawake wafundishwe kujikubali na kujiamini kwa sasababu wakiamua wanaweza na wakajiamini hakuna hata mwanamume mmoja atakayekuwa mbunge,” amesema Njenda.

Akizungumzia masuala ya uongozi shirikishi, Mkurugenzi wa Shirika lililo la kiserikali la Binti Makini, Janeth John amesema kuwa jamii yote inapaswa kushirikishwa katika uamuzi wa masuala yanayowahusu kuanzia ngazi chini ili kuwawezesha kutoa vipaumbele vyao katika masuala yanayowahusu.

“Uongozi shirikishi ni kuanzia kwenye familia au wewe unaishia kuambiwa hiki kijiko ni chako ila mashamba ni ya baba, je tunashirikishwa au tunabaki kuwa wamiliki wa masufuria. Tukutane pamoja tuangalie huu uongozi shirikishi utunufaishe sisi sote,” amesema Janeth.

Janeth ameongeza kuwa uongozi shirikishi ni chachu ya usawa na kwamba ikiwa hakuna uongozi shirikishi utakosekana wanawake wataendelea kuchakazwa na shughuli za mashambani.

“Kama wanawake hawashirikishwi kwenye kuuza wanawake tutabaki kuwa vibarua na kwenye kilimo, wanaume wamekuwa wana mtazamo hasi wanasema unawamchia mwanamke akauze il akanunue nguo, vipodozi,” ameongeza Janeth.

Kwa upande wake Mratibu wa Kituo cha Maendeleo ya Watoto na Vijana wa Kanisa la Kiinjili Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Pare kwa Ushirika na Compassion, Giliard Mkumbwa amesema ili kuwezesha kuwapo usawa katika jamii ni lazima wanaume wafundishwe kuhusu malezi ili kuwajengea uwezo wa kulea watoto tangu wakiwa wadogo.

“Tuwekeze kwenye malezi mtoto wa kiume afundishwe tangu akiwa mdogo kuwezesha mtoto wa kike anapata nafasi ya kucheza. Wanawake mna uwezo wa kuamua nani awe mbunge au Rais, kwa sababu ya wingi wenu lakini kuna jambo la kudharauliana mwanamke mwenzenu anapogombea nafasi yoyote,” amesema Mkumbwa.

Mkazi wa Kijiji cha Vumari Matongo wilayani Same, Naye mshiriki wa warsha hiyo Marijani Maziray alisema baadhi ya wanawake wametawaliwa na hofu na kuamini kuwa masuala ya uongozi yanawahusu wanaume pekee huku akisisitiza kuendelea kutolewa elimu zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles