28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

‘WANAWAKE WANAOUGUA MAGONJWA YA FIGO HUSHINDWA KUSHIKA MIMBA’

Na Veronica Romwald, Dar es Salaam

Wanawake wanaougua magonjwa ya figo hukabiliana na matatizo ya uzazi hasa kushindwa kushika mimba na hata kuharibika kwa mimba.

Kutokana na hali madaktari hulazimika kuwasaidia kukomaza mtoto iwapo mjamzito amekaribia kipindi cha kujifungua lakini pia kwa hali hiyo husababisha wengi huzaa mtoto njiti.

Daktari Bingwa wa Magonjwa wa Wanawake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk. Vincent Tarimo amesema hayo jana alipozungumza na Mtanzania Digital katika mahojiano maalumu.

“Magonjwa ya figo kwa wanawake yanaweza kuwekwa katika makundi makubwa mawili, kuna yanayohusiana na ujauzito na yasiyohusiana na ujauzito ambayo yote huweza kuua,” amesema.

Amesema katika yale yanayohusiana na ujauzito tatizo la shinikizo la juu la damu ndilo ambalo huchochea zaidi figo kuathirika na kufa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles