28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

WANAWAKE WAFUNGUKA MACHUNGU YAO KWA MAKONDA

Na TUNU NASSOR-DAR ES SALAAM


WANAWAKE zaidi ya 1,000 wa Jiji la Dar es Salaam wamewashtaki wazazi wenzao kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kuwatelekeza na kushindwa kutimiza majukumu ya malezi ya watoto.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika ofisi ya Mkoa wa Dar es Salaam, wanawake hao wamedai kunyimwa fedha za matumizi ya watoto huku wenza wao wakiwatelekezea majukumu ya ulezi bila msaada wowote.

Mmoja wa wanawake hao Mkazi wa Salasala , Habiba Hassan ambaye ni mama wa watoto wawili alidai mumewe, Mohamed Mchopa aliondoka nyumbani zaidi ya miaka 10 na kumwachia watoto ambao hadi sasa anahangaika nao kuwalea.

Alisema anafanya biashara ya kuuza chapati ili aweze kuwalisha wanawe na kumudu gharama za maisha ikiwamo nauli za shule za watoto.

“Aliondoka mwaka 2007 na kuniachia watoto wawili ambao nimehangaika kuwalea mpaka sasa mmoja anamaliza kidato cha nne na mwingine yupo kidato cha kwanza,” alisema Habiba.

Aliongeza kuwa mzazi mwenzie alirudi mwaka 2014 kwa lengo la kuuza nyumba aliyokuwa akiishi lakini yeye alikataa.

“Akaleta mteja nikakataa, akanishitaki mahakamani, tukiwa bado na kesi alileta mabaunsa wakavunja nyumba hivyo nikalazimika kwenda kupanga nyumba jirani,” alisema Habiba.

Naye mkazi wa Mbagala, Faidha Mohamed alisema alikuwa anaishi na mzazi mwenzake aliyemtaja kwa jina la Mohamed Said ambaye ni mwendesha bodaboda.

Alisema mzazi mwenzie huyo alikuwa anakesha usiku kucha akirudi anamwachia Sh 1,000 kwa ajili ya matumizi ya siku nzima.

“Nikimwambia fedha anayoniachia haitoshi anasema tusifuatiliane ikabidi niondoke kutafuta hifadhi kwa rafiki,” alisema Faidha.

Alisema aliamua kwenda Ustawi wa Jamii kushtaki ambapo mzazi mwenzake huyo alikamatwa na kupelekwa mahakamani.

“Aliamriwa kunipa Shilingi 60,000 kila mwisho wa mwezi lakini fedha hizo alizitoa kwa muda wa miezi mitatu, uliofuata akatoa sh 45,000 na baadaye akasema hawezi kunihudumia na wanangu,” alisema

Faidha ambaye ni mama wa mapacha wawili alisema aliporudi ustawi wa jamii aliambiwa akakate rufaa mahakamani jambo ambalo lilikuwa gumu kwake.

“Nilivyosikia tangazo la kuja huku nikaona ni afadhali huenda nikapata msaada wa matunzo ya wanangu,” alisema Faidha.

Naye mkazi wa Changanyikeni, Grace Mtweve alisema alikuwa anaishi na mzazi mwenzie ambaye walizaa naye mtoto wa miaka mitatu.

Alisema baadaye mzazi mwenzie huyo alimwambia kuwa yeye (Grace) anamtia mikosi kwa kuwa hapati fedha kila akitoka kutafuta.

 

Kwa habari zaidi jipatie nakala ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles