25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Wanawake 7,600 wakeketwa Singida

MWANDISHI WETU – SINGIDA

JUMLA ya wanawake na watoto 7,648 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida wamekeketwa katika kipindi cha kuanzia mwaka 2016 na 2018.

Hayo yalielezwa juzi mjini hapa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Save the Mother and Children of Central Tanzania (SMCCT), Evalyene Lyimo katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa utetezi dhidi ya mila potofu ya ukeketaji na udhalilishaji uliofanyika Ikungi hivi karibuni.

 “Kuanzia Januari hadi mwezi Oktoba 2018 jumla ya wanafunzi 37 wa shule ya sekondari wilayani humo walibainika kuwa na mimba, huku wanawake na watoto 7,648 wakiwa wamekeketwa katika kipindi cha mwaka 2016 hadi 2018,” alisema Lyimo.

Akizungumzia mradi huo, Lyimo alisema ulianza mwaka juzi hadi mwaka jana na kuwa katika kipindi hicho umetoa elimu juu ya madhara yatokanayo na mila potofu na udhalilishaji wa kijinsia kwa wakazi wapatao 15,000.

Akichangia hoja katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Edward Mpogolo, aliwata viongozi wa madhehebu ya dini na mangariba wastaafu kushiriki kikamilifu vita dhidi ya vitendo hivyo.

Alisema utekelezaji wa masuala ya mila kwa mambo ya maendeleo ni jambo jema, lakini inapokuwa kinyume kama masuala hayo ya ukeketaji, inakuwa ni changamoto kubwa kwa jamii, pia ni kinyume na haki za binadamu.

“Tuna taarifa kuwa ukeketaji wa sasa wanafanyiwa watoto wadogo na wachanga ambao hawawezi kukataa au kujihami na vitendo hivyo.

“Serikali haitaweza kuvumilia kuona vitendo hivyo vikiendelea na mtu yeyote atakayebaanika anavifanya atachukuliwa hatua kali,” alisema Mpogolo. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles