25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaume wanyonya maziwa ya wake zao kukata kilevi

Na FRANCIS GODWIN-IRINGA 

BAADHI ya wanaume wametajwa kuwa na tabia ya kunyonya maziwa ya wake kwa ajili ya kukata kilevi, wameonywa kuacha kufanya hivyo kwani humaliza lishe bora kwa watoto.

Hoja hiyo imeibuka jana katika kongamano la lishe Mkoa wa Iringa lililoandaliwa na Asasi isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na masuala ya kijamii ikiwemo Lishe Bora ya Tanzania Home Economics Association (TAHEA-Iringa), ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM, Queen Mlozi.

Alisema zipo sababu mbalimbali zimekuwa zikitajwa ikiwamo tabia kwa baadhi ya wanaume wanaolewa kupindukia kufikia hatua ya kunyonya maziwa ya mama anayenyonyesha kwa imani ya kukata pombe jambo ambalo si sawa kwani hawawatendei haki watoto ambao wanastahili kunyonya maziwa hayo kama lishe bora.

Alisema kuwa wanaume wenye tabia hizo wanapaswa kubadilika kwani Mkoa wa Iringa umekuwa ukisikika kwa kuwa na hali hiyo, ingawa ulevi upo katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema wakati mapambano dhidi ya lishe yakiendelea nchini ila bado kuna haja ya kuendelea kutoa elimu kwa jamii kama  ili kutomaliza lishe ya watoto kwa kunyonya maziwa ya mama anayenyonyesha

Pamoja na hali hiyo Mlozi alikemea tabia kwa baadhi ya wanawake ambao wamekuwa wakiwapa pombe watoto ili wao waweze kulala au kuendelea na majukumu yao jambo ambalo ni kinyume na utaratibu wa malezi.

Katibu Mkuu huyo wa UWT,  alisema ni wakati wa TAHEA kuendeleza mapambano dhidi ya lishe bora kwani bado kuna haja ya mkakati huo kuchukuliwa na mikoa yote kuona umuhimu wa elimu bora ya lishe bora ambayo watoto wanapaswa kupewa.

Alisema ni jambo la kusikitisha kwamba wakati hali hiyo ikiendelea lakini bado takwimu zinaotaja mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe kwa kuongoza kuwa na utapiamlo kwa watoto licha ya kuwa ni mikoa yenye uzalishaji mkubwa wa vyakula.

“Kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya Mwenyekiti wetu wa UWT Mama Gaudentia Kabaka naomba nikupongeze sana Mjumbe wetu wa Baraza Taifa, Lediana Mng’ong’o kwa kazi nzuri unayoifanya ndani ya Mkoa wa Iringa, maana mambo makubwa na mazuri umekuwa ukiyafanya kwa maana sisi tuliposema tunawaita wewe ulikuwa umekwishaanza kwa sababu si kitu rahisi kufungua ofisi zinazozingumzia masuala ya lishe ndani ya mikoa 21 Tanzania, sisi tunatambua kazi yako kubwa nawe ni hazina kubwa kwa nchi yetu,” alisema Mlozi

Licha ya hali hiyo pia alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi kwa kushirikiana na Katibu Tawala wake, Happines Seneda katika harakati za kuunga mkono jitihada za lishe bora kwenye mkoa huo ambapo aliwaomba wazidishe mapambano hayo kwa masilahi ya jamii.

Awali wakizungumza katika kongamano hilo Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Iringa, Nicolina Lulandala,  alisema  TAHEA imeonyesha njia kwa kila kundi kwa kufanyakazi ya elimu ya lishe kwa jamii.

Akizungumzia hali ya lishe kwa Mkoa wa Iringa, Mng’ong’o alisema kuwa hali ya lishe si nzuri na inapaswa elimu kutolewa zaidi .

Alisema hali ya lishe ya watoto kwa Iringa ni asilimia 71, Mufindi 58, Kilolo 39  huku kiwango cha matumizi ya pombe kwa wanawake wanaonyonyesha  kikiwa ni asilimia 28, Kilolo 30 na Mufindi 38.

Alisema madhara ya pombe ni pamoja na kupelekea kudharaulika, kupunguza hamu ya kula, inaleta magonjwa ya ngozi .

“Hali hii pia husababisha uvivu na kupunguza umakini katika kazi, ajali na vifo vitokanavyo na ajali , watoto wachanga kulaliwa hadi kufa na wazazi wao wakiwa wamelew,” alisema 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles