Arodia Peter, Dodoma
Wanaume wanaopigwa, kunyanyaswa kingono na wake zao na ukatili mwingine wametakiwa kuripoti matukio hayo katika madawati ya jinsia yaliyopo vituo vya Polisi nchini.
Wito huo umetolewa na bungeni leo Mei 2, na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Faustine Ndugulile wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Mkoa wa Iringa, Rita Kabati (CCM).
Katika swali lake Kabati aliuliza: Kwakuwa vitendo vya wanaume kupigwa , kunyanyaswa na wake zao vimeongezeka ni lini serikali italeta sheria ili kuwalinda wanaume hao?
Katika majibu yake, Dk. Ndugulile amesema sheria ya ukatili wa kijinsia haibagui nani amefanyiwa ukatili huo kati ya wanaume na wanawake, hivyo wanaume wanaopigwa na kufanyiwa vitendo vyovyote vya ukatili waripoti madawati ya jinsia yaliyopo vituo vya polisi.