31.7 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

WANAUME WALALAMIKA KUNYANYASWA NA WAKE ZAO

ALLY BADI- LINDI

BAADHI ya wanaume wa Kata  ya  Kilolambwani wilayani  Lindi wamelalamika kuteswa na wake zao kwa kuwashurutisha kufanya kazi kinyume na imani za dini.

Wakizungumza kwa niaba  ya wenzao kwenye utambulisho wa mradi wa usawa na jinsia jana, walisema tangu mashirika na asasi za raia zianze kutoa elimu kuhusu haki za wanawake na watoto tabia za wake zao zimebadilika.

Mmoja wa wanaume hao, Farijala Mchopa, alisema elimu inayotolewa na mashirika hayo inakwenda kinyume na imani ya dini zao na hivi sasa wanawake hao hawatawaliki kinyume na matakwa ya dini yao.

Mchopa  alishauri asasi inayoratibu mafunzo hayo, Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake na Watoto cha Lindi (LIWOPAC) na shirika la kimataifa la misaada la OXFA, kuhamasisha zaidi    watu wafunge ndoa za serikali  usawa unaohubiriwa uweze kukamilika na  kukubalika  kwa pande  zote.

“Usawa huu ili ukubalike, mashirika haya yahamasishe kuanza mchakato wa kuanzisha vyama na mashirika ya kutetea haki za wanaume   na kuchangishana mahali,”alisema Mchopa.

Msimamizi wa mradi huo, Romana Colman, licha ya kueleza lengo la mradi huo, alisema asasi za  iraia ikiwamo LIWOPAC hazina nia ya kufarakanisha jamii bali haki na usawa ndiyo msingi wa amani na utulivu katika jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles