24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

WANAUME WAKACHA UPIMAJI UKIMWI

Na FRANCIS GODWIN, IRINGA


WAKATI  Mkoa wa Iringa ukianza kampeni ya miezi sita ya upimaji wa Virusi vya Ukimwi kupitia ‘Furaha yangu pima, jitambue, ishi’, imeelezwa kuwa wanaume wengi mkoani hapa hawana tabia ya kupima Ukimwi huku wengine wakituma wake zao kwa ajili ya kupima pindi wanapokuwa wajawazito.

Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Wilaya ya Mundi, Jamhuri Willaim ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Amina Masenza, kwenye uzinduzi wa kampeni hiyo uliofanyika Mwembetongwa mjini hapa.

Alisema takwimu zinaonyesha wanaume zaidi ya 18,416 ndio ambao wanatumia dawa za ARV kwa ajili ya  kufubaza  makali ya  VVU, wakati wanawake wakiongoza kwa kutumia  dawa hizo za ARV kwa kufikia wanawake  34847 kuwa  takwimu   hizo  zinaonyesha  wanaume  wengi bado hawajapima  kujua hali zao  na kuanza matumizi ya tiba.

Alisema takwimu hizo zinaonyesha wanawake ndio wanaojitokeza kupima VVU wakati wanaume wakiwa nyuma na kupitia kampeni hiyo, mkoa unakusudia kupima watu 90,000.

“Kampeni hii ya kupima VVU na kuanza  kutumia tiba  ya ARV mapema,  tunaomba wanaume  wote  kujitokeza  na  wananchi  wengine wote,” alisema DC Wiliam.

Alisema baada ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia mpango wa kitaifa wa kudhibiti Ukimwi kwa  kushirikiana na  TACAIDS  na  wadau  wa  USAID  kuja na kampeni ya Furaha yangu mjini Dodoma, Mkoa wa Iringa nao walijipanga kwa ajili ya kampeni hiyo.

Awali Mbunge wa Viti Maalumu wa Mkoa wa Iringa, Ritta Kabati (CCM), aliwataka wanawake  kuwahamasisha  waume  zao  kwenda  kupima kwani kuendelea  kuwatumia  wanawake  kupima kwa niaba  yao  maambukizi ya  Ukimwi hayatapungua mkoani  hapa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles