31.2 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Wanaume asilimia 49 wabambikiwa watoto

Dad-PyramidRuth Mkeni, Dar es Salaam

ASILIMIA 49 ya matokeo ya uchunguzi wa Makosa ya Vinasaba (DNA) yanayowasilishwa katika ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa mwaka, yanaonesha kuwa baba si mzazi halali wa mtoto.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samweli Manyele, alisema asilimia 100 ya sampuli zinazofikishwa ofisini kwake kwa ajili ya uchunguzi zinaonesha kiwango hicho kuwa baba anayedhaniwa siye.

“Kesi zinazopelekwa katika maabara yetu zinahusu sampuli ya vinasaba. Kwa mwaka zinaonesha kuwa asilimia 49 kati ya asilimia 100 ya matokeo hayo mzazi mmoja ambaye ni baba kuwa si mzazi halali wa mtoto huyo.

“Vinasaba ni utambulisho wa kipekee wa kila kiumbe ambao unabeba taarifa muhimu inayorithisha tabia au umbile fulani la mhusika. Vinasaba ni kama vile kitabu cha kumbukumbu kinachohusu maisha binafsi,” alisema.

Kuhusu sheria alisema. “Tunaposimamia sheria ya vinasaba vya binadamu kama wakala wa maabara ya mkemia mkuu tunazingatia sana sheria na kwa kufanikisha hilo kitu cha kwanza sheria inatambua nani anaruhusiwa kuleta sampuli, nani anatakiwa kuchukua sampuli na kuzifikisha katika maabara yetu.

“Lakini pia sheria hii inaagiza mara baada ya vipimo kufanyika ni nani anatakiwa kupewa majibu. Kwa mfano mtu binafsi ana sampuli zake anahitaji zichunguzwe tunafanya kazi yake na kumpa majibu yake, lakini kipimo kile anachofanya yeye hawezi kukitumia katika maamuzi ya kisheria,”alisema Profesa Manyele.

Alisema ili mtu huyo aweze kutumia kipimo hicho katika uamuzi wa kisheria endapo atamshirikisha mwanasheria.

“Hii maana yake ni kwamba aliyeleta sampuli hizo aziwakilishe kwa wakili, kwa kuwa yeye ndiye anastahili kupata majibu na kumfikishia muhusika kwa kufuata sheria,”alisema.

Aidha watu wanaostahili kuomba vipimo vya DNA katika ofisi yao ni pamoja na mahakama, Jeshi la Polisi na hospitali.

Profesa Manyele alisema kesi za DNA pekee ni 200 hadi 300 kwa mwaka, huku akitaja mikoa inayoongoza kuwa ni ile ya Kanda ya Ziwa, Dar es Salaam, Mbeya na Arusha.

Kuhusu mkutano huo, Profesa Manyele alisema unalengo la ni kuimarisha uhusiano uliopo kati ya wadau wa kemikali na wadau wa afya ya mazingira kutoka katika halmashauri mbalimbali nchini.

Aidha alibainisha kuwa baadhi ya majukumu yanayofanywa na ofisi yake ni pamoja na kufanya uchunguzi ili kuhakiki ubora na usalama wa vyakula, dawa, maji, maji machafu, bidhaa za viwanda na mashambani, sampuli za mazingira na sampuli zinazohusiana na makosa ya jinai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles