31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Wanasiasa hawataki kukosolewa- Askofu Niwemugizi

Na Clara Matimo, Ngara

ASKOFU wa Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge- Ngara, Severine Niwemugizi, amesema licha ya wanasiasa wengi kutopenda kukosolewa wanapofanya mambo yaliyokinyume na matakwa ya Mungu, lakini  viongozi wa dini  hawana budi kutumia karama zao kuwakosoa na kuwarejesha Katika mstari.

Padri Godfrey Baraka Rusasa, akiwa amelala kifudifudi ikiwa ni ishara ya kujitoa kwa Mungu ili kuwachunga kondoo wake.

Alitoa kauli hiyo Juni 9, mwaka huu wakati akimpa daraja takatifu la upadri Shemasi Godfrey Baraka Rusasa, katika kanisa la Mtakatifu Fransisco wa Asis  lililopo Ngara mjini Mkoani Kagera ambapo alimtaka kutumia nafasi hiyo kuwakosoa watu wa makundi yote wakiwemo wanasiasa wanapokengeuka.

Alisema  viongozi wa dini wanatumwa na Mungu kama Nabii Ezekiel alivyotumwa kwenda kwa watu waliomuasi kuwaambia juu ya maasi yao hawajitumi hivyo wasiogope kundi lolote kuliambia linapoasi juu ya uasi wao na Bwana atawalinda.

“Wanasiasa wanataka watende  mambo ya ufedhuli fedhuli lakini tusiwakemee nenda kaponye majeraha  ya watu wanaoumizwa, unakwenda kwenye nyumba ya waasi, kundi la mbwa mwitu watakushambulia ili unyamaze usiogope maana Bwana Mungu amekutuma usiwaogope, usichukuliwe na malimwengu, usinunuliwe.

“Siku zote wanasiasa hawapendi kukosolewa, huwa wanatukemea tunapowaambia ukweli kuhusu uasi wao sisi wengine midomo yetu iliishakula kiapo cha kusimamia ukweli huwa tunawakemea  wanapotenda mambo yanayokwenda kinyume na haki za watu ingawa baadhi yao wanaweza kukuzushia mambo ya uongo lakini usiogope maneno yao,  usiwaogope wala usifadhaike,” alisema na kuongeza.

“Leo utatumwa kama Nabii Ezekiel alivyotumwa kwenda kwa watu waliomuasi Mungu, utageuza mkate na divai kuwa damu na mwili wa Kristo Bwana amekutuma uwaambia watu wake yale yasiyofaa wayaache, padri ni daraja la utumishi ujikane nafsi kwa ajili ya huduma ya watu wengine,  Mungu alisema anayewapokea ananipokea mimi lakini anayewakataa amenikataa mimi,” alisema Askofu Niwemugizi.

NAMI NI PADRI:Askofu wa Kanisa katoliki Jimbo la Rulenge;Ngara, Severine Niwemugizi (mwenye kofia)  akiwa katika picha ya pamoja na mapadri wa kanisa hilo kutoka nchi mbalimbali waliofika kushuhudia upadrisho wa  Padri Godfrey Baraka Rusasa mwenye nguo nyeupe anayefuata baada ya askofu huyo.

Aidha Askofu Niwemugizi alitoa rai kwa wazazi , walezi kuwajibika katika malezi ya watoto wao ikiwemo kuwapa majina mazuri kama Baraka na mengine ya Mitume na sio Sikujua, Matatizo na Mateso huku wakiwafundisha mafundsho ya Mungu ili kanisa liendelee kupata makuhani wengi maana  mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache ndani ya shamba la Mungu.

Akizungumza baada ya Misa ya shukrani iliyofanyika nyumbani kwao Mtaa wa Nakatunga Juni 10, 2022, Padri Godfrey Baraka Rusasa, aliwataka waumini wa dhehebu lake kutenda kama Mungu alivyoagiza katika Biblia Takatifu Isaya 1:17 isemayo jifunzeni kutenda mema, takeni hukumu na haki, wasaidieni walioonewa huku akiwaahidi kuwatumikia kwa moyo wake wote pamoja na kuwaombea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles