25 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 6, 2022

Contact us: [email protected]

Wanasheria waijadili Escrow siku ya tatu

George Masaju
George Masaju

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM

UAMUZI wa Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Kibiashara (ICSID), kulitaka Shirila la Umeme Tanzania (Tanesco) kuilipa Benki ya Standard Chartered ya Hong Kong (SCB-HK) Dola za Marekani milioni 148.4  umeendelea kuwaumizi vichwa wanasheria wa upande wa utetezi, ambapo kwa siku ya tatu mfululizo wanapitia hukumu hiyo.

Jopo hilo la wanasheria hao waliongozwa na Wanasheria wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, pamoja na timu ya wanasheria waliokuwa wakiiwakilisha Tanesco katika shauri hilo  ambao mawakili wa kampuni za R.K Rweyongeza & Advocates na Crax Law Partners

Taarifa za ndani zililiambia MTANZANIA kuwa hukumu hiyo inaonekana ni mwiba, ambapo jopo hilo sasa linaangalia namna ya kuinasua Tanesco ili kukwepa kulipa fedha hizo ambazo ni zaidi ya Sh bilioni 320.

“Hukumu hii inaelekea kuchanganya kidogo maana na jopo la wataalamu wa sheria chini ya Mwanasheri Mkuu wa Serikali pamoja na wale waliokuwa wanaitetea Tanesco jangu juzi (majuzi) wanajifungia kuangalia namna ya kupangua hoja.

“Lakini kinachochanganya katika hili ni kwamba sijui itakuwa maana uamuzi wa Mahakama ya ICSID haupingwi katika chombo chochote ingawa huenda timu hii ya mangwiji wa sheria wanaweza kutoka na alau na watu tunaelekea katika suala hili zito,” kilisema chanzo hicho cha ndani kutoka serikalini.

Wakati jopo hili likikuna vichwa upande wa Tanesco kupitia kwa Mkurugenzi wake Mkuu, Felchesmi Mramba, alinukuliwa na gazeti moja la kila siku (si MTANZANIA) akisema kwa sasa wanasubiri ushauri wa timu hiyo ya wanasheria wao ndiyo watakuwa na la kusema ni hatua gani wanachukua.

Zitto alia na JPM

Kutokana na sakata hilo Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo)  alimwomba Rais Dk. John  Magufuli kuonyesha hasira zake  kwa kile alichodai ufisadi mkongwe wa IPTL.

“Nimesoma ‘arbitral award’’ ambayo Benki ya Standard Chartered wametunukiwa na ICSID ( Case no. ARB/10/20) na kuumizwa sana kutokana na kwamba hoja zote ambazo zimetumika kuwapa ushindi SCB ndizo Kamati ya PAC (wakati huo) ilizijenga kwenye taarifa yake maalumu iliyopitishwa na Bunge na kutolewa maazimio manane .

“Ndio hoja hizo hizo zilibezwa na Serikali chini ya Waziri Sospeter Muhongo na umma kuambiwa kuwa Tanesco hawatakuwa na madai dhidi yao.

“Mahakama hii ( tribunal ) ya ICSID imethibitisha maonyo ya PAC kwamba hasara kwa nchi kwenye kashfa ya Tegeta Escrow itakuwa ni mara mbili ya fedha zilizochotwa kwani mwenye mali akijulikana tutapaswa kumlipa tena,” alisema Zitto na kuongeza.

“Tulimpa Harbinder Singh Seth Shilingi bilioni 306 na tunapaswa kuwalipa SCB Shilingi bilioni 320. Jumla shilingi bilioni 626. Na bado tunamlipa Seth kila mwezi dola milioni 4 kwa umeme wa mtambo alioupata kitapeli,” alisema.

Kutokana na hali hiyo alisema kuwa Mahakama ya ICSID imesema IPTL ni mali ya Benki ya Standard Chartered, ambapo alimuomba Rais Magufuli kuliona jambo hilo kwani ana fursa ya kihistoria kumaliza kabisa kile alichokiita  mtandao wa wizi na utapeli uliodumu tangu mwaka 1995.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,606FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles