30 C
Dar es Salaam
Monday, September 27, 2021

Wanasayansi kufanya jaribio

LONDON, Uingereza

WANASAYANSI wanatarajiwa kufanya majaribio ya dawa kuona kama inaweza kuzuia kuganda kwa damu kunakohusishwa na ugonjwa wa Covid-19.

Majaribio hayo, yaliyofadhiliwa na wakfu wa British Heart yataangazia dhana ya kuwa mgando wa damu unasababishwa na kutosawazika kwa homoni kunakotonaka na maambukizi ya virusi vya corona.

Hiyo itakuwa moja ya dawa ambayo inafanyiwa majaribio ya kuzuia athari mbaya za ugonjwa wa Covid-29.

Theluthi moja ya wagonjwa waliolazwa kwasababu ya virusi vya corona, damu yao huganda na kuwaweka katika hatari zaidi.

Dawa  ya TRV027, inafanya kazi ya kurekebisha homoni na kuziweka sawa zenye kuhusishwa na shinikizo la juu la damu, maji na chumvi

Wanasayansi wa Chuo cha Imperial College London, wanaofanya majaribio hayo, wanafikiria kwamba virusi vinaingia ndani ya mwili, na kutumia kimeng’enya kama njia ya kuingia kwenye seli.

Lakini dawa hiyo,  inafanya kimeng’enya kutofanya kazi na kuwa na jukumu muhimu katika kusawazisha homoni za msingi. Homoni inapokuwa hivyo, damu inaweza kuanza kunata na kusababisha mgando.

Ilikuwa chanzo cha aliyeibuna kushinda tuzo ya Nobel – inaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kurekebisha homoni.

Tiba nyingi ambazo zinafanyiwa majaribio ya kutibu ugonjwa wa huo, zinazingatia zaidi kukabiliana na kufura kwa mwili.

“Lakini kutosawazika kwa homoni ni tatizo kubwa ambalo linaweza kutoa kidokezo katika suala la kwanini watu wengine huumwa sana wakipata Covid-19 tofauti na wengine, alisema Dk. David Owen,.

Tangu ulipobainika  ugonjwa wa Covid-19 unaathiri sehemu nyingi za mwili, tiba hii inaweza kutumiwa kwa pamoja na dawa nyengine amesema Dkt. Kat Pollock, kulingana na utafiti ulifanywa awali.

  Pia imesemekana usalama kwa wagonjwa wenye matatizo ya moyo ingawa haikuwa yenye ufanisi ilipotumika kama tiba katika ugonjwa wa Covid-19.

Dawa ya TRV027 ni moja tu kati ya kadhaa zinazofanyiwa majaribio kupunguza makali ya athari au kusaidia mwili kukabiliana na virusi hivyo.

Takriban dawa 10 za kukabiliana na virusi ikiwemo ile ya HIV lopinavir/ritonavir zinafanyiwa majaribio au zishafanyiwa majaribio kuangalia ikiwa zinaweza kusaidia katika makabiliano dhidi ya ugonjwa huu.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,352FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles