23.1 C
Dar es Salaam
Sunday, September 8, 2024

Contact us: [email protected]

Wanariadha wa Olimpiki wang’ara Africa Day Marathon

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Wanariadha wa maarufu Tanzania na wale walifuzu kushiriki michezo ya Olimpiki, wameng’ara na kubeba katika mbio za Africa Day Marathon zilizofanyika leo Mei 18, 2024 jijini Dar es Salaam.

Wanariadha hao ni Alphonce Simbu (JWTZ)aliyebuka mshindi wa kwanza katika mbio za kilomita 15, akikimbia kwa dakika 42:56, wa pili ni John Welle(Talent Arusha) amekimbia dakika 43:11 na namba tatu imekwenda kwa Faraja Damas(JWTZ) aliyekimbia dakika 43:29.

Kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza kilomita 15 ni Jackline Juma alikimbia kwa dakika 48:36, wa pili Magdalena Shauri ametumia dakika 48:54 wote wa JWTZ, wa tatu ni Sara Ramadhan kutoka Arusha amemaliza na dakika 49:25.

Katika mbio hizo za kilomita 5 na 15, zimehusisha
mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zao hapa nchini na wanariadha wakongwe Filbert Bayi na Juma Ikanga.

Akizungumzia ushindi huo, Simbu amesema ni moja ya sehemu ya kujipima kutokana na mazoezi wanayofanya ambapo wakirejea mazoezini watajua ni wapi waanzie na kama mwanariadha anayetarajia kushiriki mashindano makubwa ya Olimpic ni muhimu kupata mbio za ndani.

“Nimejisikia furaha kushiriki mbio hizi za Africa Day, hii ni kama jaribio kuangalia mazoezi yamefikia wapi. Niwapongeze waandaaji ukiangalia mbio imekuwa na usalama tofauti na mbio nyingine tunanyang’ana barabara na magari,” amesema Simbu.

Mgeni rasmi katika mbio hizo, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amesema watahakikisha mbio hizo zinakuwa na mafanikio makubwa.

“Mwaka huu 2024 Umoja wa Afrika(AU), umetimiza miaka 61 tangu kuanzishwa kwake. Tumepata mafanikio makubwa kiuchumi, kisiasa, Ulinzi na Usalama, ni muhimu tuendeleze mshikamano wetu tuweze kutimiza ndoto zetu na za waasisi wetu ili kufikia Afrika tunayoitaka”, amesema Balozi Mbarouk.

Naye Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Wakili Jackson Ndaweka, ameishukuru Wizara kwa kuchagua mchezo wa riadha kuwa katika maadhimisho hayo na wamefanikiwa kumepata washiriki wengi kutokana na kwamba riadha mtu yoyote anaweza kushiriki.

“Kwa niaba ya Shirikisho la Riadha Tanzania, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Wizara kuweza kuchagua mchezo wa riadha, najua ipo michezo mingi ingeweza kuwepo. Tumepokea kwa heshima kubwa na tunaomba ushirikiano huu uendelee,” amesema Ndaweka.

Kwa upande wake mkongwe wa riadha Filbert Bayi, amewapongeza wanariadha wa Tanzania kukubali kwenda kushirikiana na mabalozi katika siku hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles