25.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Wanaokaimishana vyeo kitanzini

RENATHA KIPAKA-BIHARAMULO

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Umma na Utawala Bora, Dk. Mary Mwanjelwa, amewataka watumishi kufuata sheria taratibu za kazi ya umma kwa kutekeleza miongozo inayotolewa na Serikali.

Alisema hayo jana wilayani Biharamulo mkoani Kagera, baada ya kupokea taarifa ya utumishi na utawala iliyosomwa na Mkuu wa Wilaya, Saada Malunde.

Dk. Mwanjelwa alisema katika utumishi, suala la sababu binafsi lenye kufanya kupeana madaraka ya kukaimu nafasi ambayo haina mhusika, ni kuvunja mioyo ya kazi kwa watumishi wengine.

Alisema Serikali ilitoa waraka mwaka 2018 ambao unatamka juu ya nafasi ambazo hazina wakuu wa idara zinapaswa kukaimiwa ndani ya miezi sita, endapo kuna sababu ya kuendelea itolewe  taarifa.

“Waraka ulitolewa tayari wenye kurasa nyingi, nafasi zote zisiwe zaidi ya miezi sita, endapo mnaona kuna sababu toeni taarifa, acheni kupendekezana, fanyeni uwajibikaji,” alisema Dk. Mwanjelwa.

Alisema taarifa ya wilaya imeonyesha kuna watumishi wamekaimu nafasi zaidi ya mwaka mmoja kwenye idara ya ardhi, fedha, maendeleo ya jamii na afya bila kufanya uamuzi wowote.

Dk. Mwanjelwa alisema kukaimu muda mrefu kunafanya mhusika wa nafasi ile kushindwa kuona ufanisi wa kazi yake juu ya ukaimishwaji nafasi ambayo amepangiwa na mwajiri wake.

Alisema kufanya hivyo kunatokana na mazoea kazini, bila kutambua uwajibikaji.

“Jamani awamu hii siyo ya mazoea, fanyeni uwajibikaji, tambueni haki kila mmoja wetu, acheni upendeleo, ndani ya kazi hatuhitaji hayo, tuangalie nidhamu, weledi na ubunifu,” alisema Dk. Mwanjelwa.  

Alisema upandishwaji wa madaraja umeshatolewa nchi nzima, tayari nafasi 193,000 zimetangazwa na watumishi wenye sifa na viwango vya elimu ya juu watapandishwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,211FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles