Na Mwandishi Wetu, Morogoro
Makundi hatarishi yakiwemo wanaofanya ngono kinyume na maumbile, wanaotumia madawa ya kulevya na wale wanaofanya biashara ya ngono yametajwa kuwa kwenye hatari kubwa ya maambukizi UKIMWI.
Hayo yamebainishwa leo Januari 26, mkoani Morogoro na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, kwenye ufunguzi wa Warsha ya Watekelezaji wa Afua za UKIMWI kwa fedha za mzunguko wa kwanza wa mfuko wa Kili Challenge.
Dk. Maboko amesema UKIMWI bado ni tatizo kubwa kijamii na kiuchumi kwa Watanzania kutokana na kuendelea kuwapo kwa maambukizi mengi hasa kwa makundi hatarishi.
“Ndugu washiriki wa warsha, UKIMWI bado ni tatizo kubvva kijamii na kiuchumi kwa watanzania kwa ujumIa, bado kuna maambukizi mengi kwa watanzania wenzetu wailioko kwenye makundi hatarishi kama wale wanaofanya ngono kinyume cha maumbile, wanaotumia madawa ya kulevya na wale wanaofanya biashara ya ngono.
“Makundi mengine ambayo yameathirika na pia yamo kwenye hatari kubwa ya kupata maambukizi ya UKIMWI ni pamoja na madereva wa malori yaendayo masafa marefu, wafanyakazi wa kwenye mashamba makubwa na jamii,” amesema Dk. Maboko.
Aidha, ameyataja makundi mengine kuwa ni pamoja na wanaofanyakazi za uvuvi na migodini.
Amesema takwimu zinaonesha kwamba kundi la vijana wadogo waliopo kati ya miaka 15-24 ndiyo limeathirika zaidi hususan vijana wa kike.
“Hivyo makundi haya hatarishi yanahitaji mikakati maalumu ya kuzuia maambukizo mapya ya VVU kwao na kwa jamii kwa ujumla.
“Hivyo tume kwa kushirikiana na Mgodi wa dhhabu wa Geita(GGM) tunaendelea naujenzi na uboreshaji wa vituo vya maarifa ambavyo vinatoa huduma za mapambano ya dhidiya ukimwi kwa makundi tajwa hapo juu,” amesema Dk. Maboko.
Amefafanua kuwa vituo hivyo vimekuwa na manufaa hususan kuongeza kasi ya utoaji wa huduma kwa jamii.
Akitolea mfano mwaka 2020 amesema kuwa kituo cha Dumila kilichoko mkoani humo kilianza kutoa huduma kwa wasafirishaji wa masafa marefu na jamii ya Dumila na kufanya jumla ya vituo kufikia vine vinavyotoa huduma kupitia programu hiyo.
“Vituo vingine ni Geita, Mchungwani (Handeni), na Manyoni mkoani Singida, katika mzunguko wa kwanza wa programu hii mfuko umeweza kusaidia Asasi za kiraia 20 ambazo zinapatiwa jumla ya Sh milioni 543.6 zikijumhisha mikoa 11 na Halmashauri 15 zinatarajiwa kunufaika kwenye awamu hiyo ya utekelezaji.
“Aidha, katika awamu hiyo ya kwanza maeneo yaliyopewa kipaumbele ni pamoja na huduma na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU, huduma za kinga, elimuya masuala ya afya kwa vijana.
“Pia kuna misaada kwa watoto walio katika mazingira magumu, kupambana na unyanyapaa na ubaguzi, kutoa elimu kwa watoa huduma majumbani na elimu ya matumizi sahihi ya dawa za kufubaza VVU miongoni mwa waviu,” amesema Dk. Maboko.
Amesema kwa Mkoa wa Geita programu hii imewezesha Kituo cha watoto yatima (Moyo wa Huruma) kuendelea kulea na kusomesha watoto yatima walioachwa na wazazi wao kutokana na janga hili la Ukimwi.
Pia katika Mkoa wa Arusha kikundi cha kina Mama wafugaji wa Ng’ombe wa maziwa (Arusha Pastoral Women Counsel) wameweza kuboresha shughuli zao za ufugaji kupitia progamu hii, ambapo kwa sasa wanafuga kwa njia ya kisasa ambayo imepelekea kupata mapato makubwa ikilinganishwa na awali.
“Aidha, program hii imeongeza weledi uelewa wa wananchi katika mapambano dhidi ya UKIMWI kupitia mafunzo mbalimbali yaliyokuwa yanatolewa na Asasi katika Mikoa ya Lindi, Kagera, Ruvuma, Iringa, Morogoro, Kagera, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Pwani, Dar es Salaam na Kilimanjaro.
“Mfumo huu wa utoaji fedha kwa kuzishindanisha Asasi mbalimbali kutokana na ubora wa maandiko ndiyo umeanza kwa mzunguko wa kwanza ambapo Asasi hizi 20 zimeandaa mandiko bora zaidi miongoni ma waombaji 264 waliowasilisha maandko.
“Jambo la msingi hapa ni kuongeza uwazi na ubora wa maandiko ambapo matarajio ya Serikali kupitia TACAIDS na GGM ni kuona taasisi zilizopewa fedha zinatekeleza kwa ufanisi nakuhakikisha fedha zinawafikia walengwa huku malengo yaliyokusudiwa yakifikiwa,” amesema Dk. Maboko na kuongeze kuwa:
“Malengo makubwa ya mpango mkakati wa kitaifa wakudhibiti UKIMWI wa awamu ya nne ni kuiwezesha serikali kuimatisha programu za kuzuia maambukizi mapya, kutoa huduma za tiba ya magonjwa nyemelezi, kupunguza athari za ugonjwa wa UKIMWI kwenye jamii na Taifa kwa ujumla.
“Pia kujenga mazingira bora ya utekelezaji wa mpango wa kuzuia maambukizo mapya ya VVU nchani ikiwa ni pamoja na yale ya kutoka kwa mama kwenda kwa rntoto pamoja na kupunguza maambukizo kwa wasichana balee na wanawake nchini,” amesema.