29.1 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 20, 2024

Contact us: [email protected]

Wanandoa wauawa kwa kuchinjwa

Na  Walter  Mguluchuma-Katavi

HUU ni nyama. Ndivyo unavyoweza kusema, baada ya wana ndoa, Noel  Anthony Mswanya(39) na mkewe Stella Noel  (39)  wakazi wa Mtaa wa Migazini Kata ya Nselwa Manispaa ya  Mpanda, kuuawa kikatili kwa kuchinjwa kama kuku.

Kabla ya kuchinjwa, wana ndoa hao walichomwa vifu sehemu mbalimbali za miili yao wakiwa wamelala ndani ya nyumba yao.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Leonald Makona  alisema  tukio hilo  lilitokea Desemba 15, mwaka huu saa 7 usiku wakiwa wamelala.

Alisema kabla ya mauaji  hayo,wanandoa hao walikuwa wamelalala ndani ya nyumba, ghala mlango wa nyumba yao ulivunjwa kwa kutumia jiwe kubwa maarufu (fatuma) na watu wasiojulikana.

Alisema baada ya kuvunja, watu hao waliingia ndani ya chumba walichokuwa wamelala na kuanza kuawashambulia.

“Baada ya kuingia chumbani walianza kumshambulia  mwanaume kwa kumchoma visu sehemu mbalimbali za mwili wake, huku mkewe akiangalia, licha kupiga yowe  kuomba msaada kwa majirani, wauaji  hawakujari,’alisema.

Alisema baada kumchinja shingo mwanaume, wauaji hao ambao hawajahamika idadi yao, walianza kumshambulia mke wa marehemu, licha ya kukimbia nje ya nyuma, huku akipiga yowe kuomba msaada wa majirani .

Alisema wauaji  waliamkimbiza na kumkamata akiwa umbali wa mita 50 kutoka  nyumbani kwake.

“Baada ya kumkamata walimrudisha hadi  ndani, kisha wakamuua kwa kumchinja kikatili,”alisema.

Alisema  majirani  waliwashuhudia wauaji hao kwa kuwachungulia kupitia madirisha ya nyumba zao, lakini walishindwa kujitokeza kuwasaidia.

Alisema majirani hawakuwatambua wauaji kutokana na kuwa tochi zenye mwanga mkali.

“Wengi wao walihofia kutoka nje, maana wangeweza kuuawa, tukio hili limetushtua tunalifanyia kazi,”alisema.

Alisema mpaka sasa, jeshi hilo linaendelea na uchunguzi na msako mkali  dhidi ya wauaaji hao ili kuwakamata.

Aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo ili kufanikisha msako huo .

Miili ya marehemu wote, imehifadhiwa  Hospitali ya Mkoa wa Katavi kwa ajiri ya uchunguzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles