26.7 C
Dar es Salaam
Thursday, November 14, 2024

Contact us: [email protected]

Wananchi wazuia msafara wa mkuu wa mkoa

NA IBRAHIM YASSIN, SONGWE

WAKAZI wa Kibaoni Kata ya Kapalala wilayani Songwe mkoani Songwe wamezuia msafara Mkuu wa Mkoa huo, Brigedia Jenerali, Nickodemas Mwangela wakitaka  asikilize kero zao .

Kesro hizo ni pamoja na kuchomewa nyumba, kutozwa fedha za kiingilio huku wakitakiwa kuondoka kwenye eneo hilo kwa madai kuwa ni hifadhi ya wanyamapori.

Baada ya msafara huo kusimama, Brigedia Jenerali Mwangela alimtaka Ofisa wa Maliasili na Wanyamapori wa mkoa huo, Abdallah Mgonja kueleza uhalali wa wananchi kuishi eneo hilo   na kuwatoza fedha.

Katika maelezo yake, Mgonja alisema   awali wananchi hao ambao tayari wamejenga nyumba katika eneo hilo walielezwa wazi kwamba hapafai kuishi kwa sababu  ni hifadhi ya wanayamapori ambao hupita katika hifadhi hiyo kwenda maeneo mengine.

Baada ya maelezo hayo, Brigedia Mwangela aliwataka wananchi kueleza ukweli endapo walitoa rushwa na kupewa maeneo hayo  hatua za sheria ziweze kufuatwa.

Mmoja wa wakazi wa Kibaoni, Mageta Maduhu alisema walipohitaji kuhamia katika eneo hilo Serikali ya kijiji iliwatoza fedha kati ya Sh 50,000 hadi Sh 100,000 kwa kila mtu mmoja lakini wameshangaa viongozi wa wilaya   waliwavamia na kuwachomea nyumba zao.

Ester Mkamba mkazi wa Kapalala alisema walihamia eneo hilo baada ya kutozwa fedha hizo na kusema kuwa endapo eneo hilo ni hifadhi uongozi wa serikali ya kijiji wasingewatoza fedha na badala yake wangewaeleza wahamie maeneo mengine.

”Mkuu wa mkoa, sisi tupo hapa baada ya kuruhusiwa na serikali ya kijiji, tumelipa fedha na tunachangia nguvu kazi na fedha katika shughuli za maendeleo kwa sasa tumelima mazao na tunaishi kwa amani,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles