29.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 17, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Wananchi watakiwa kulipa kodi kwa hiari ili kusaidia maendeleo

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Wananchi wametakiwa kuendelea kulipa kodi kwa hiari ili kuiwezesha serikali kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta za maji, afya, elimu na huduma nyingine za jamii.

Wito huo umetolewa leo Ijumaa Februari 14, 2025, jijini Dodoma na Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Francis Kaunda, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Shukrani kwa Mlipa Kodi, yaliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Dodoma.

Sherehe hizo zilihusisha matembezi ya hiari kutoka ofisi za TRA kupitia mitaa mbalimbali hadi Uwanja wa Jamhuri na kumalizika kwa hafla fupi iliyojumuisha wateja wa mamlaka hiyo.

Kaunda amesisitiza kuwa ulipaji wa kodi ni jukumu la kila mwananchi na kuhimiza TRA kuendelea kutoa elimu ili kuongeza mwamko wa wananchi kulipa kodi kwa hiari.

“TRA ina jukumu la kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi. Serikali yetu itaendelea kutekeleza miradi mikubwa endapo wananchi wataendelea kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi,” amesema.

Naye Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Pendolake Elinisafi, amesema mamlaka hiyo inaendelea kuboresha huduma kwa wateja ili kurahisisha ulipaji wa kodi bila shuruti.

“Siku hii inatupa fursa ya kujadili changamoto zinazowakabili walipa kodi na kuzitafutia ufumbuzi. Ni matumaini yetu kuwa elimu ya kodi itaendelea kutolewa kwa wigo mpana zaidi,” amesema Elinisafi.

Maadhimisho hayo yamelenga kuhamasisha wananchi kuhusu umuhimu wa kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
595,000SubscribersSubscribe

Latest Articles